Luka 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Matangulizi.

1Wengi walijaribu kuandika masimulio ya mambo yale yaliyotimilika kwetu.

2Waliyafuatafuata yale waliyoambiwa na wenye kuyaona yote kwa macho yao, yalivyokuwa tangu mwanzo, kwani walikuwa wamelitumikia lile Neno.

3Sasa nami nimeyafuata na kuyachungua yote mpaka hapo, yalipoanzia, nikaona, inafaa, nikuandikie sawasawa, kama yalivyofuatana, mwenzangu Teofilo,Wimbo wa Maria.

46Maria akasema:

Bwana ndiye, moyo wangu unayemkuza,

47roho yangu humshangilia Mungu, mwokozi wangu.

48Maana ameutazama unyenyekevu wa kijakazi wake;

kwani tokea sasa itakuwa, wao wa vizazi vyote wanishangilie.

49Amenifanyia makuu kwa kuwa mnguvu, Jina lake ni

takatifu.

50Huruma yake huwajia vizazi kwa vizazi wamwogopao.

51Hufanya ya nguvu kwa mkono wake

akiwatawanya waliojikweza katika mawazo ya mioyo yao.

52Huangusha wenye nguvu katika viti vya kifalme,

lakini wao walio wanyenyekevu huwapandisha.

53Walio wenye njaa huwashibisha mema,

lakini wenye mali huwaacha, wajiendee mikono mitupu.

54Alipokumbuka huruma, akamsaidia mtoto wake Isiraeli,

55kama alivyowaambia baba zetu, akina Aburahamu

nao walio uzao wake kwamba: Wawe wa kale na kale!

56Maria akakaa kwake, yapata miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake.

Kuzaliwa kwake Yohana.

57Elisabeti siku zake za kuzaa zilipotimia, akazaa mtoto mume.

58Majirani zake na ndugu zake waliposikia, ya kuwa Bwana amemwonea huruma nyingi, wakafurahi pamoja naye.

59Ilipokuwa siku ya nane, wakaja kumtahiri mtoto, wakamwita jina la baba yake: Zakaria.

80Yule mtoto alipokua akapata nguvu Rohoni, akakaa nyikani mpaka siku, alipowatokea Waisiraeli.*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help