1Hivyo mlivyo naye Kristo, nawabembeleza kwamba: Ikiwa mwatulizana mioyo kwa kupendana, ikiwa m wenye roho moja, au ikiwa m wenye mioyo ya kuoneana uchungu na huruma,
2ikiwa hivyo, itimilizeni furaha yangu, mawazo yenu yakiwa yayo hayo ya kupendana kila mtu na mwenziwe, mioyo ikiwa mmoja tu wa kulitaka neno lili hili la kwamba:
3Pasifanyike jambo lolote kwa kuchokozana wala kwa kujitakia majivuno ya bure, ila mnyenyekeane kila mtu akimwazia mwenziwe kuwa mkubwa kuliko yeye!
5*Mioyoni mwenu myawaze yaleyale, Kristo Yesu aliyoyawaza!Timoteo na Epafurodito.
19Namngojea Bwana Yesu, aitikie, nimtume Timoteo upesi kwenu, moyo wangu upate kutulia ukitambua, mambo yenu yalivyo.
20Kwani sinaye mtu mwingine, tuliyepatana naye mioyo kama huyu; naye huyasumbukia kweli mambo yenu.1 Kor. 16:10.
21Kwani wote huyafuata yaliyo yao; hawayafuati yaliyo yake Kristo Yesu.2 Tim. 4:10,16.
22Lakini yeye mmemtambua, ya kuwa ni mwelekevu, kwani kama mtoto anavyomtumikia baba yake, vivyo hivyo ameitumikia kazi ya kuutangaza Utume mwema pamoja nami.
23Nangojea, nipate kumtuma yeye; itakuwa papo hapo, nitakapoona, mambo yangu yatakavyotimilika.Fil. 1:12.
24Hili nalo nalishika moyoni kwamba: Bwana atanipa nami kuja upesi kwenu.Fil. 1:25.
25Lakini nalishurutishwa moyoni kumtuma Epafurodito kwenu; yeye ni ndugu na mwenzangu wa kazi na wa vita; kisha ni mtume wenu anayenipatia yenye kunitunza.Fil. 4:18.
26Akawa akiwatunukia ninyi nyote, akasikitika sana, kwa sababu mlikuwa mmesikia, ya kuwa aliugua.
27Naye alikuwa mgonjwa kweli, kufa kukamfikia. Lakini Mungu akamhurumia, tena siye yeye tu, ila mimi nami, masikitiko yasifuatane kwangu mimi.
28Kwa hiyo nimemtuma upesiupesi, mpate kuonana naye na kufurahi tena, nami masikitiko yanipungukie.
29Kwa hiyo mpokeeni katika Bwana kwa furaha yote! Nao walio hivyo wapeni macheo!1 Kor. 16:16.
30Kwani kwa ajili ya kazi ya Kristo alijifikisha kufani, asijitunzie mwenyewe, akitaka kunifanyizia kazi zote za utumishi, ambazo hamkuweza kunifanyizia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.