3 Mose 23 - Swahili Roehl Bible 1937

Siku ya mapumziko.

1Bwana akamwambia Mose kwamba:

2Sema na wana wa Isiraeli ukiwaambia: Sikukuu za Bwana, mtakazozitangaza kuwa za kukutania Patakatifu, hizo sikukuu zangu ndizo hizi:

3Kazi sharti zifanywe siku sita, lakini siku ya saba ni siku ya kupumzika kabisa ya kukutania Patakatifu; hapo isifanywe kazi yo yote, maana ndiyo siku ya mapumziko ya kumheshimu Bwana katika makao yenu yote.Sikukuu ya Pasaka.

4Hizi ndizo sikukuu za Bwana za kukutania Patakatifu, nanyi sharti mzitangaze, siku zao zilizowekwa zitakapotimia:Mwaka mpya.

23Bwana akamwambia Mose kwamba:

37Hizi ndizo sikukuu za Bwana, ndipo mtangaze, watu wakutanie Patakatifu kumtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa: za kuteketezwa nzima pamoja na vilaji vya tambiko, tena ng'ombe za tambiko za kuchinjwa pamoja na vinywaji vya tambiko, kila moja siku yake, kama siku inavyopaswa.

38Lakini tena ziko siku za mapumziko za Bwana na vipaji, mnavyovitoa wenyewe, hata vipaji, mnavyovitoa kwa kuyalipa mliyoyaapa, na vipaji vinginevingine, mnavyomtolea Bwana kwa kupendezwa mioyoni.

39Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mapato ya nchi, sharti mle sikukuu ya Bwna siku saba, siku ya kwanza ni ya mapumziko, nayo ya nane ni ya mapumziko.

40Tena siku ya kwanza na mjipatie matunda mazuri ya miti na makuti mabichi ya mitende na matawi ya miti ya maporini na ya mitoni, mmfurahie Bwana Mungu wenu siku saba.Neh. 8:14-16.

41Siku hiyo iliyo sikukuu ya Bwana sharti mwile kila mwaka siku saba. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu, mwile sikukuu hii siku saba.

42Na mkae vibandani siku saba, wote walio wenyeji kwao Waisiraeli na wakae vibandani.

43Ni kwa kwamba vizazi vyenu wajue, ya kuwa niliwakalisha vibandani nilipowatoa katika nchi ya Misri. Mimi Bwana ni Mungu wenu.

44Mose akawaambia wana wa Isiraeli hizo sikukuu za Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help