2 Samweli 14 - Swahili Roehl Bible 1937

Yoabu anatumia mwanamke wa Tekoa kumpatia Abisalomu upole kwa Dawidi.

1Yoabu, mwana wa Seruya, alipotambua, ya kuwa moyo wa mfalme umerudi kumwelekea Abisalomu,

2Yoabu akatuma Tekoa kumchukua huko mwanamke aliye mwerevu wa kweli, akamwambia: Jitendekeze kuwa mwenye kufiwa, ukivaa nguo za matanga pasipo kujipaka mafuta, uwe sawasawa na mwanamke anayemlilia mfu siku nyingi.

3Kisha uende kwa mfalme, mwambie maneno kama haya! Naye Yoabu akamwambia, atakayoyasema na kinywa chake.

4Basi, huyo mwanamke wa Tekoa akaja kusema na mfalme akijiangusha chini kifudifudi, kwamba amwangukie, akasema: Nisaidie, mfalme!

5Mfalme alipomwuliza: Una nini? akasema: Mimi ni mwanamke mjane kweli, maana mume wangu amekufa.

6Tena kijakazi wako alikuwa na wana wawili wa kiume, nao wakagombana shambani; kwa kuwa hakuwako aliyewaamua, mmoja akampiga ndugu yake, mpaka akamwua.

7Mara ukoo wote ukamwinukia kijakazi wako na kusema: Mtoe aliyempiga ndugu yake, tumwue kwa ajili ya roho ya ndugu yake, aliyemwua, tumtoweshe naye atakayelichukua fungu lake! Ndivyo, wanavyotaka kulizima nalo kaa la mwisho lililosalia, wasimwachie mume wangu huku nchini jina wala sao lo lote.

28Abisalomu alipokaa Yerusalemu miaka miwili pasipo kuonana na mfalme uso kwa uso,

29ndipo, Abisalomu alipotuma kwa Yoabu, apate kumtuma kwa mfalme, lakini akakataa kufika kwake. Akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kufika.

30Ndipo, alipowaambia watumishi wake: Tazameni, liko shamba la Yoabu linalopakana na langu, nalo ni la mawele yake. Nendeni, mlichome moto! Ndipo, watumishi wa Abisalomu walipolichoma moto hilo shamba.

31Ndipo, Yoabu alipoondoka, akaja kwa Abisalomu nyumbani kwake, akamwuliza: Mbona watumishi wako wamelichoma shamba langu moto?

32Abisalomu akamjibu Yoabu: Tazama, nalituma kwako kwamba: Njoo hapa, nikutume kwa mfalme kumwambia: Mbona nimekuja na kutoka Gesuri? Ingenifaa, nikae huko bado. Lakini sasa na nitokee usoni pake mfalme, kama ziko manza, nilizozikora, basi, na aniue.

33Yoabu alipokwenda kwa mfalme kumpasha hizi habari, akamwita Abisalomu; naye alipofika kwa mfalme akamwangukia mfalme na kujiangusha chini kifudifudi, ndipo, mfalme alipomnonea Abisalomu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help