1 Mose 40 - Swahili Roehl Bible 1937

Yosefu anafumbua ndoto za wafungwa.

1Ikawa, mambo hayo yalipomalizika, mkuu wa watunza vinywaji vya mfalme wa Misri na mkuu wa wachoma mikate wakamkosea bwana wao, mfalme wa Misri.

2Naye Farao akawakasirikia hawa watumishi wake wawili wa nyumbani mwake, Yule mkuu wa watunza vinywaji naye mkuu wa wachoma mikate.

3Akawafunga, waangaliwe kifungoni katika nyumba ya mkuu wao waliomlinda mfalme; ndimo, Yosefu alimokuwa naye kwa kufungwa.

16Mkuu wa wachoma mikate alipoona, ya kuwa amefumbua vema, akamwambia Yosefu: Mimi nami katika ndoto yangu nimejiona, nilipokuwa nimechukua nyungo tatu zenye vikate vyeupe kichwani pangu.

17Namo katika ungo wa juu vilikuwamo vikate vizuri vyo vyote vya Farao, wachoma mikate wanavyovitengeneza, nao ndege wakavila mwenye ungo kichwani pangu.

18Yosefu akajibu akisema: Maana yake ndio hii: hizo nyungo tatu ndio siku tatu;

19siku tatu zitakapopita, Farao atakupa kukiinua kichwa chako, kiwe juu yako zaidi, atakunyonga katika mti, nao ndege watazila nyama za mwili wako.

Ndoto zao wale wafungwa zinatimia, kama Yosefu alivyosema.

20Siku ya tatu ikawa siku ya kuzaliwa kwake Farao; ndipo, alipowaandalia watumishi wake wote karamu; hapo katikati ya watumishi wake akampa mkuu wa watunza vinywaji naye mkuu wa wachoma mikate kuviinua vichwa vyao,

21akimrudisha mkuu wa watunza vinywaji katika kazi yake ya kutunza vinywaji, ampe Farao kikombe mkononi mwake,

22naye mkuu wa wachoma mikate akamnyonga, kama Yosefu alivyowafumbulia ndoto.

23Lakini mkuu wa watunza vinywaji hakumkumbuka Yosefu, akamsahau.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help