1Hizikia akatuma kwa Waisiraeli na kwa Wayuda wote, nao Waefuraimu na Wamanase akawaandikia barua, waje Yerusalemu Nyumbani mwa Bwana Mungu wa Isiraeli kula sikukuu ya Pasaka ya Bwana Mungu wa Isiraeli.
23Kisha mkutano wote ukafanya shauri kuendelea siku saba tena, wakala sikukuu tena siku saba kwa furaha.
24Kwani Hizikia, mfalme wa Wayuda, aliutolea huo mkutano madume ya ng'ombe 1000 na mbuzi na kondoo 7000, nao wakuu waliutolea mkutano madume ya ng'ombe 1000 na mbuzi na kondoo 7000; nao watambikaji walijieua wengi.2 Mambo 35:7.
25Wakafurahi watu wote wa huo mkutano wa Wayuda pamoja na watambikaji na Walawi na mkutano wao wote waliotoka kwa Waisiraeli nao wageni waliotoka katika nchi ya Waisiraeli nao waliokaa katika nchi ya Wayuda.
26Ikawa furaha kubwa mle Yerusalemu, kwani tangu siku za Salomo, mwana wa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli, haya kuwamo mle Yerusalemu mambo kama hayo.
27Mwisho watambikaji na Walawi wakainuka, wakawabariki watu; sauti zao zikasikiwa, nayo maombo yao yakafika mbinguni kwenye Kao lake takatifu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.