Luka 9 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuwatuma mitume.(1-6: Mat. 10:1,7,9-11,14; Mar. 6:7-13.)

1Akawaita wale kumi na wawili, wakusanyike, akawapa uwezo na nguvu za kufukuza pepo wote na za kuponya magonjwa.

2Akawatuma, wautangaze ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.

3Akawaambia: Msichukue kitu cha njiani, wala fimbo wala mkoba wala chakula wala shilingi, tena mtu asiwe na nguo mbili!

4Nyumbani mo mote mtakamoingia, kaeni humo! Namo ndimo, mtakamotoka tena!Kujiokoa.

23Akawaambia wote: Mtu akitaka kunifuata mimi ajikataze mapenzi yake, ajitwishe kila siku nao msalaba wake, kisha anifuate!Mkubwa ni nani?(46-50: Mat. 18:1-5; Mar. 9:33-40.)

46Wakawa wakiwaza mioyoni mwao kwamba: Aliye mkuu kwetu ni nani?

47Lakini Yesu akayajua, waliyoyawaza mioyoni mwao, akatwaa kitoto, akamsimamisha kando yake,

48akawaambia: Mtu atakayempokea kitoto huyu kwa Jina langu hunipokea mimi. Tena akinipokea mimi humpokea yule aliyenituma mimi. Kwani aliye mdogo kwenu ninyi wote, huyo ndiye mkuu.Wasamaria wanamkataa Yesu.

51*Ikawa, zilipotimia siku zake za kuchukuliwa mbinguni, mwenyewe akauelekeza uso kwenda Yerusalemu,

52akatanguliza wajumbe mbele yake. Hao walipokwenda, kuingia kijiji cha Wasamaria, wamtengenezee mahali,

53hawakumpokea, kwani uso wake ulikuwa umeelekea kwenda Yerusalemu.

54Wanafunzi akina Yakobo na Yohana walipoviona wakasema: Bwana, wataka, tuseme, moto ushuke toka mbinguni, uwamalize, kama Elia naye alivyofanya?

55Lakini akapinduka, akawatisha akiwaambia: Hamjui, kama m wenye Roho gani?

56Mwana wa mtu hakujia kuangamiza roho za watu, ila kuziokoa. Kisha wakaenda zao, wakafikia kijiji kingine.*

Kumfuata Yesu.(57-60: Mat. 8,19-22.)

57Walipokuwa wakienda njiani, palikuwapo aliyemwambia: Nitakufuata po pote, utakapokwenda.

58Yesu akamwambia: Mbweha wanayo mapango, nao ndege wa angani wanavyo vituo, lakini Mwana wa mtu hana pa kukilazia kichwa chake.

59Alipomwambia mtu mwingine akasema: Nifuate! huyo akasema: Nipe ruhusa, kwanza niende nimzike baba yangu!

60Naye akamwambia: Waache wafu, wazike wao kwa wao! Lakini wewe nenda, uutangaze ufalme wa Mungu!

61Mtu mwingine akasema: Nitakufuata, Bwana, lakini kwanza nipe ruhusa, niwaage waliomo nyumbani mwangu!

62Yesu akamwambia: Mtu ashikaye jembe mkononi na kuvitazama vya nyumba, huyo hatauweza ufalme wa Mungu.*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help