2 Mambo 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Mweuo wa Nyumba ya Mungu.(Taz. 1 Fal. 7:51—8:11.)

1Kazi zote, ambazo Salomo aliifanyia nyumba ya Bwana zilipomalizika, Salomo akavipeleka vipaji vitakatifu vyote vya baba yake Dawidi pamoja na fedha na dhahabu na vyombo vyote, akaviweka penye vilimbiko vya nyumba ya Mungu.

2Kisha Salomo akawakusanya wazee wa Waisiraeli nao wote waliokuwa vichwa vya mashina nao wakuu wa milango ya wana wa Isiraeli mle Yerusalemu kwenda kulitoa Sanduku la Agano la Bwana katika mji wa Dawidi ulioitwa Sioni.

3Ndipo, watu wote wa Isiraeli walipkusanyika kwa mfalme kufanya sikukuu, ikawa mwezi wa saba.

11Kisha watambikaji wakatoka Patakatifu; nao hawa watambikaji waliooneka hapo walikuwa wamejitakasa wote pasipo kuziangalia zamu zao,

12nao waimbaji wote pia walio Walawi, wale wa Asafu na wa Hemani na wa Yedutuni pamoja na wana wao na ndugu zao, wote walikuwa wamevaa nguo za bafta, wakashika patu na mapango na mazeze, wakawa wamesimama upande wa maawioni kwa jua penye meza ya kutambikia, tena walikuwako pamoja na watambikaji 120 wenye kupiga matarumbeta.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help