Mashangilio 100 - Swahili Roehl Bible 1937

Kumshukuru Mungu na kupaingia Patakatifu pake.Wimbo wa kushukuru.

1Mpigieni Bwana shangwe, nchi zote! Mtumikieni Bwana na kufurahi!

2Tokeeni mbele yake na kupiga shangwe!

3Tambueni, ya kuwa aliye Mungu ndiye yeye Bwana! Yeye ndiye aliyetufanya, sio sisi wenyewe, tu watu wa ukoo wake na kondoo wa malishoni pake.

4Ingieni milangoni mwake na kumshukuru! Ziingieni nyua zake na kumshangilia! Mshukuruni! Nalo Jina lake likuzeni sana!

5Kwani Bwana ni mwema, nao upole wake ni wa kale na kale, nao welekevu wake ni wa vizazi na vizazi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help