Matendo ya Mitume 15 - Swahili Roehl Bible 1937

Mkutano wa mitume.

1Kulikuwa na watu waliotelemka toka Yudea, wakaja huko, wakawafundisha ndugu kwamba: Hamwezi kuokoka msipotahiriwa, kama Mose alivyotuzoeza.

16Hayo yakiisha, nitarudi, nikijenge tena

kibanda cha Dawidi kilichoanguka;

hapo palipojenguka nitapajenga tena, nipate kukisimamisha

tena,

17maana watu waliosalia wote wapate kumtafuta Bwana

pamoja na wamizimu wote waliotangaziwa Jina langu.

Ndivyo, asemavyo Bwana anayeyafanya haya.

18Yanatambulikana toka kale.

19Kwa hiyo mimi naona: Wanaotoka kwa wamizimu na kumgeukia Mungu tusiwachukuze mizigo isiyofaa,

20ila tuwaandikie kwamba: Miiko ni hii tu: Kutambikia mizimu, maana huchafua moyo wa mtu, tena ugoni, tena nyamafu, tena damu.Barua ya mitume.

22Ndipo, mitume na wazee walipopatana na wateule wote kuchagua wenzao wengineo na kuwatuma kwenda Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba. Wakamchagua Yuda anayeitwa Barsaba na Sila, waliojua kuongoza ndugu.

23Wakaandika barua, waipeleke mikononi mwao, ni ya kwamba: Sisi mitume na wazee tunawaamkia kindugu ninyi ndugu zetu huko Antiokia na Ushami na Kilikia mliotoka kwa wamizimu.

24Tumesikia, ya kuwa wengine watu, tusiowaagiza neno, wamewahangaisha kwa maneno ya kuwatia wasiwasi mioyoni mwenu.Tume. 15:1.

25Tukakusanyika kwa hivyo, tulivyo na moyo mmoja, tukapatana kuchagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wenzetu akina Barnaba na Paulo, tunawapenda,

26kwani ni watu waliojitoka wenyewe kwa ajili ya Jina la Bwana wetu Yesu Kristo.

27Basi, tumemtuma Yuda na Sila, nao watawaelezea kwa vinywa maneno yaya haya.

28Kwani sisi na Roho Mtakatifu tumepatana, tusiwatwike mzigo kuliko yaleyale yanayofaa,

29mshike mzio wa nyama za tambiko na wa damu na wa nyamafu na wa ugoni. Mkijikataza mambo haya mtafanya vema. Kaeni vema! Salamu.

30Kisha wakasindikizwa, wakatelemka kwenda Antiokia, wakawakusanya wao wote wa hilo kundi, wakawatolea ile barua.

31Wale walipoisoma wakafurahi kwa ajili ya matulizo.

32Hata Yuda na Sila waliokuwa wafumbuaji wenyewe wakawatuliza ndugu na kuwaambia mengi, wakawashupaza.Tume. 11:27; 13:1.

33Walipokwisha kukaa kitambo walisindikizwa na ndugu kwa hivyo, walivyopatana, warudi kwao waliowatuma.

34Lakini Sila alipendezwa kukaa huko.

35Naye Paulo na Barnaba wakakaa Antiokia wakilifundisha Neno la Bwana na kuipiga hiyo mbiu njema pamoja na wenzao wengi.

36Siku zilipopita, Paulo akamwambia Barnaba: Turudi tena, tuwakague ndugu mijini mote, tulimolitangaza Neno la Bwana!1 Tes. 3:5.

37Lakini Barnaba alitaka kumchukua naye Yohana aliyeitwa Marko.Tume. 12:12,25.

38Lakini Paulo alidhani, haifai kumchukua aliyewatoroka huko Pamfilia, asifuatane nao kazini.Tume. 13:13.

39Kwa hiyo wakabishana kwa ukali, hata wakatengana yeye na mwenziwe; Barnaba akamchukua Marko, akaingia chomboni kwenda Kipuro,

40naye Paulo akamchukua Sila, akaondoka akiombewa na ndugu, Mungu awaongoze kwa upole.

41Akaipita nchi ya Ushami na Kilikia, akawashupaza wateule.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help