Ezekieli 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Mapatilizo ya wakuu wa Yuda.

1Roho ikanichukua, ikanipeleka kwenye lango la Nyumba ya Bwana la mashariki lielekealo maawioni kwa jua. Hapo pa kulilingilia lile lango nikapaona waume 25; katikati yao nikamwona Yazania, mwana wa Azuri, na Pelatia, mwana wa Benaya, walio wakuu wa ukoo huu.Matulizo ya roho zao waliotekwa.

14Neno la Bwana likanijia la kwamba:

15Mwana wa mtu, ndugu zako, hawa ndugu zako, ambao mlitekwa pamoja nao, hata mlango wote wa Isiraeli, hawa wote ndio, wenyeji wa Yerusalemu waliowaambia: Nendeni mbali mkitoka kwake Bwana! Sisi tumepewa nchi hii, iwe yetu!

16Kwa hiyo sema: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema kwamba: Kweli nimewapeleka mbali kwenye wamizimu na kuwatawanya katika hizo nchi siku hizi zilizo chache, nikawa mwenyewe patakatifu pao katika nchi hizo, walikopelewa.Ez. 6:8-10; Yer. 24:5-6.

17Kwa hiyo sema: Hivi ndivyo Bwana Mungu anavyosema: Nitawakusanya ninyi na kuwatoa katika hayo makabila, kweli nitawaunganisha ninyi na kuwatoa katika nchi hizo, nilikowatawanya, niwape ninyi nchi ya Isiraeli.Yer. 29:14.

18Napo watakapoiingia watayaondoa huko matapisho yake yote na machukizo yake yote.

19Nami nitawapa kuwa moyo mmoja, tena nitatia roho moja mioyoni mwao; namo miilini mwao nitaitoa mioyo iliyo migumu kama mawe nikiwatia mioyo inayolegea kama nyama.Ez. 36:26; Yer. 24:7.

20Ndivyo, watakavyoyafuata maongozi yangu na kuyashika mashauri yangu, wayafanye. Watakuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wao.Yer. 31:33.

21Lakini wenye mioyo iyaelekeayo matapisho yao na machukizo yao, mioyo yao ikayafuata, basi, nitawapatilizia njia zao vichwani pao.

22Ndipo, Makerubi walipoyakunjua mabawa yao, nayo magurudumu yakawa kando yao, nao utukufu wa Mungu wa Isiraeli ukawa juu yao.Ez. 1:4-28.

23Kisha utukufu wa Bwana ukapanda ukiondoka mle mjini katikati, ukasimama juu ya mlima ulioko karibu ya mji upande wa maawioni kwa jua.

24Roho ikanichukua, ikanipeleka katika nchi ya Wakasidi kwenye mateka kwa nguvu ya hayo maono ya Roho ya Mungu. Kisha hayo maono, niliyoyaona, yakaniondokea.Ez. 3:12.

25Nikawaambia waliotekwa mambo yote ya Bwana, aliyonionyesha.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help