2 Mambo 13 - Swahili Roehl Bible 1937

Abia anamshinda Yeroboamu.(Taz. 1 Fal. 15:1-8.)

1Katika mwaka wa 18 wa mfalme Yeroboamu Abia akapata kuwa mfalme wa Wayuda.

2Akawa mfalme mle Yerusalemu miaka 3; jina la mama yake ni Mikaya, binti urieli wa Gibeoni. Naye akapiga vita na Yeroboamu.

3Abia akajifunga kwenda vitani mwenye vikosi vya mafundi wa vita, watu 400000 waliochaguliwa. Naye Yeroboamu akajipanga vitani mwenye watu 800000 waliochaguliwa kwa kuwa mafundi wa vita wenye nguvu.

4Abia akaondoka kuja kusimama juu ya mlima wa Semaraimu ulioko milimani kwa Efuraimu, akasema: Nisikilizeni, Yeroboamu nanyi Waisiraeli wote!

5Je? Hamjui, ya kuwa Bwana Mungu wa Isiraeli alimpa Dawidi kuwa mfalme wa Waisiraeli kale na kale, yeye na wanawe, alipofanya naye agano la chumvi?

13Lakini Yeroboamu alikuwa ametuma wengine, wawazunguke, wapate kuwavizia huko nyuma kuwajia migongoni kwao; kwa hiyo wengine wao walikuwa mbele ya Wayuda, nao waliowavizia walikuwa nyuma yao.

14Wayuda walipogeuka wakaona, ya kuwa hawana budi kupigana mbele na nyuma; ndipo, walipomlilia Bwana, watambikaji wakayapiga matarumbeta yao.

15Kisha watu wa Yuda wakapiga yowe; ikawa, watu wa Yuda walipopiga yowe, Mungu akampiga Yeroboamu na Waisiraeli wote mbele ya Abia na ya Wayuda.

16Ndipo, wana wa Isiraeli walipowakimbia Wayuda, naye Mungu akawatia mikononi mwao.

17Abia na watu wake wakawapiga, pigo likawa kubwa mno; kwao Waisiraeli wakaanguka kwa kuuawa watu 500000, nao ni watu wliochaguliwa.

18Ndivyo, wana wa Isiraeli walivyonyenyekezwa siku zile, lakini wana wa Yuda wakapata nguvu, kwa kuwa walimwegemea Bwana Mungu wa baba zao.

19Abia akakimbia, amfuate Yeroboamu na kumfukuza, akateka kwake miji, ndio Beteli na mitaa yake na Yesana na mitaa yake na Efuraimu na mitaa yake.

20Yeroboamu hakupata nguvu tena katika hizo siku za Abia, kisha Bwana akampiga, akafa.

21Abia akajipatia nguvu, akajichukulia wanawake 18, akazaa wana wa kiume 22 na wa kike 16.

22Mambo mengine ya Abia na njia zake na maneno yake yameandikwa katika kitabu cha maelezo ya mfumbuaji Ido.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help