1Manase alikuwa mwenye miaka 12 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 55 mle Yerusalemu, nalo jina la mama yake ni Hefusiba.
2Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kwa kuyafuata matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Isiraeli.
3Akavijenga tena vijumba vya kutambikia vilimani, baba yake Hizikia alivyoviangamiza, akaweka nazo meza za kumtambikia Baali, akatengeneza nacho kinyago cha Ashera, kama Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, alivyofanya, akaviangukia navyo vikosi vyote vya mbinguni na kuvitumikia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.