1Kwa kuwa wako watu wanaonifokea, nihurumie Mungu! Siku zote wananigombeza na kunitesa.
5Siku zote huyabishia maneno yangu, waniumize, kwa mawazo yao yote hunitafutia mabaya.
6Wao hujikusanya, waniotee na kupanyatia, nyayo zangu zilipo, kwa sababu wanangojea kuipata roho yangu.
7Kwa ajili ya mapotovu yao hawataona wokovu, watu walio hivyo uwachafukie, Mungu, na kuwakumba!
8Siku za kutangatanga kwangu umezihesabu wewe, machozi yangu nayo yakusanye kwako katika kichupa! Najua, yamo katika kitabu chako, umeyaandika.
9Hapo, watakaporudi nyuma adui zangu, itakuwa siku ile, nitakapokuitia; maana hili ninalijua, ya kuwa Mungu yuko upande wangu.
10Kwa kuwa naye Mungu na nilitukuze Neno lake, kwa kuwa naye Bwana na nilitukuze Neno lake.
11Kwa kumwegemea Mungu sitaogopa kamwe; walio watuwatu tu wanifanyieje?
12Niliyokuapia, Mungu, nitakulipa, nikushukuru.
13Kwani umeiopoa roho yangu katika kufa; kweli, hata miguu yangu unaiangalia, isijikwae, ipate kuendelea machoni pa Mungu penye mwanga wao wenye uzima.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.