1Ndugu, hampaswi na kuandikiwa, kama itakuwa mwaka gani au siku gani, hayo yatakapokuwapo.Maonyo na salamu.
12Ndugu, twawaomba sana, mwajue wale wanaojisumbua kwenu ninyi wakiwasimamia, mkae naye Bwana, tena wakiwaonya.1 Kor. 16:18.
13Jipigieni sana kuwapa macheo na kuwapenda kwa ajili ya kazi yao! Pataneni ninyi kwa ninyi!
14*Lakini twawahimiza ninyi, ndugu: Waaonyeni wenye mambo ya ovyo tu, watulizeni wenye mioyo miepesi, wasaidieni wanyonge, wo wote waendeeni kwa uvumilivu!2 Tes. 3:15.
15Mwangalie, mtu asimlipe mwenziwe uovu kwa uovu! Ila siku zote myafuate yaliyo mema, myapatiane ninyi kwa ninyi, hata wengine wote!Fano. 20:22; Rom. 12:17,21; 1 Petr. 3:9.
16Changamkeni siku zote!Fil. 4:4.
17Mwombeni Mungu pasipo kukoma!Luk. 18:1-8; Rom. 12:12; Kol. 4:2.
18Katika mambo yote toeni shukrani! Kwani haya ndiyo, Mungu ayatakayo, myafanye, kwa kuwa wake Kristo Yesu.Ef. 5:20.
19Roho msimzime!1 Kor. 14:30,39.
20Mafumbuo msiyabeze!1 Kor. 14:1.
21Ila yote yapambanueni, kisha lishikeni lililo jema!1 Kor. 14:29; 1 Yoh. 4:1.
22Yote yaonekanayo kuwa mabaya yaepukeni!
23Lakini yeye Mungu aliye mwenye utengemano awatakase ninyi nyote miili na mioyo, kwamba roho zenu zote nzima pamoja na mioyo na miili zilindwe, zikae pasipo doadoa lo lote, mpaka Bwana wetu Yesu Kristo atakaporudi!
24Naye aliyewaita ni mwelekevu, naye ndiye atakayeyafanya.*1 Kor. 1:9; 2 Tes. 3:3.
25Ndugu, tuombeeni kwake Mungu!
26Wasalimuni ndugu wote na kunoneana, kama watakatifu walivyozoea!1 Kor. 16:20.
27Nawaapisha ninyi kwa Bwana, barua hii isomewe ndugu wote.
28Upole wa Bwana wetu Yesu Kristo uwakalie! Amin.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.