1Tengeneza nayo meza ya kuvukizia mavukizo, uitengeneze nayo kwa migunga.
2Urefu wake uwe mkono mmoja, nao upana wake uwe mkono mmoja, pande zote nne ziwe sawa, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mikono miwili.
3Uifunikize dhahabu tupu juu yake na kando yake pande zote na pembe zake, kisha uzungushe juu yake taji la dhahabu pande zote.
4Kisha uitengenezee mapete mawili ya dhahabu, uyatie chini ya taji pande zake mbili penye mbavu zake mbili, yawe ya kutilia mipiko ya kuichukulia.
5Nayo mipiko uitengeneze kwa migunga, kisha nayo uifunikize dhahabu.
6Kisha uiweke upande wa huku wa pazia linaloning'inia na kulielekea Sanduku la ushahidi, mbele ya kiti cha upozi kilichoko juu yake Sanduku la Ushahidi nitakapokutana na wewe.Mchango wa kodi.
11Bwana akamwambia Mose kwamba:
12Ukivihesabu vichwa vyao wana wa Isiraeli, watakapokaguliwa, na wamtolee Bwana makombozi ya kuzikomboa roho zao, kila mtu yake kwa kukaguliwa, wasipatwe na pigo lo lote kwa kukaguliwa.
13Kwa hiyo kila atakayefika kukaguliwa sharti atoe nusu ya sekeli, ndio fedha zitumikazo Patakatifu, ambazo sekeli moja ni gera ishirini, ndio fedha moja ya thumuni nane. Nusu ya fedha hiyo iwe kipaji cha tambiko cha kumnyanyulia Bwana.
14Kila atakayefika kukaguliwa mwenye miaka ishirini na zaidi sharti mnyanyulie Bwana hicho kipaji cha tambiko.
15Mwenye mali asilipe zaidi, wala mnyonge asiipunguze hiyo nusu ya fedha kuwa kipaji cha tambiko cha kumnyanyulia Bwana, wajipatie upozi.
16Kisha uzichukue hizo fedha za mapoza, utakazowatoza wana wa Isiraeli, uzitumie za utumishi wa hema la Mkutano; ndivyo, zitakavyokuwa za kumkumbusha Bwana, awakumbuke wana wa Isiraeli, azipatie roho zenu upozi.
Birika la shaba.17Bwana akamwambia Mose kwamba:
18Tengeneza birika la shaba lenye wekeo lake la shaba, liwe la kuogea, uliweke katikati ya Hema la Mkutano na meza ya kutambikia, kisha ulitie maji.
30Naye Haroni na wanawe uwapake mafuta, uwatakase, wapate kuwa watambikaji wangu.2 Mose 29:7.
31Nao wana wa Isiraeli uwaambie kwamba: Hayo mafuta ya kupaka sharti yawe matakatifu kwa vizazi vyenu, kwa kuwa ni yangu.
32Msiyamiminie mwilini mwa mtu, wala msitengeneze yaliyo sawa kama hayo, kwani ndiyo matakatifu, nayo sharti yawe matakatifu kwenu.
33Mtu atakayechanganya mafuta kuwa kama hayo au atakayeyapaka mtu mgeni sharti ang'olewe kwao walio ukoo wake.
Mavukizo.34Bwana akamwambia Mose: Chukua viungo vinukavyo vizuri: liwa na udi na sandarusi, ndio viungo vinukavyo vizuri, tena uvumba ulio safi, vyote viwe kipimo kimoja tu.
35Uvitengeneze kuwa mavukizo, kama mtengeneza manukato aliye fundi anavyojua kuyatengeneza na kutia chumvi humo, yapate kutakata na kuwa matakatifu.
36Kisha uchukue humo kidogo, uyaponde sana, yawe kama uvumbi, kisha uchukue humo kidogo kuyaweka mbele ya Sanduku la Ushahidi katika Hema la Mkutano, nitakamokutana na wewe. Hayo mavukizo sharti yawe kwenu matakatifu yenyewe.
37Mavukizo mengine mtakayoyatengeneza, msiyatengeneze kuwa kama hayo, ila hayo sharti yawe matakatifu kwenu kwa kuwa yake Bwana.
38Mtu atakayetengeneza mavukizo kama hayo ya kuyavukiza sharti ang'olewe kwao walio wa ukoo wake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.