1Mfalme Nebukadinesari akawaandikia makabila na koo zote, wao wote wenye ndimi za watu wanaokaa katika nchi yote nzima, kwamba: Utengemano wenu na uwe mwingi!
2Vielekezo na vioja, Mungu Alioko huko juu alivyonifanyia, imenipendeza kuvieleza.
3Vistaajabuni vielekezo vyake vilivyo vikuu! Navyo vioja vyake vilivyo vya nguvu! Ufalme wake ni ufalme wa kale na kale, nayo enzi yake ni ya vizazi na vizazi.
4Mimi Nebukadinesari nalitulia nyumbani mwangu, nikawapo na kufanikiwa katika jumba langu kuu.
5Nikaota ndoto iliyonistusha, nayo mawazo yaliyonijia, nilipolala kitandani, nayo maono ya macho yangu yakanitia woga.
6Amri ikatoka kwangu ya kuniletea wajuzi wote wa Babeli, wanijulishe maana ya ndoto.
7Kwa hiyo wakaniletea waandishi na waaguaji na Wakasidi na wachunguza nyota, mimi nikawaambia ndoto, lakini hawakunijulisha maana yake.Mfalme Nebukadinesari anaingiwa na kichaa; alipopona anamsifu Mungu.
28Hayo yote yakampata mfalme Nebukadinesari.
29miezi kumi na miwili ilipopita, siku moja alipotembea huko Babeli jumbani mwake mwa kifalme juu,
30ndipo, mfalme aliposema kwamba: Kumbe huu sio mji mkubwa wa Babeli, nilioujenga mimi kuwa kao la kifalme kwa nguvu ya uwezo wangu, utukufu wangu utukuzwe!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.