Mashangilio 75 - Swahili Roehl Bible 1937

Maamuzi yake Mungu ni ya kweli.Kwa mwimbishaji, wa kuimbisha kama wimbo wa kwamba: Usiangamize! Wimbo wa Asafu wa kushukuru.

1Twakushukuru, Mungu, twakushukuru,

2kwa kuwa Jina lako liko karibu, vioja vyako ndivyo vinavyolitangaza.

3Unasema: Itakapofika siku, niliyoiweka, mimi nitatoa maamuzi yanyokayo.

4Ijapo, nchi zitetemeke pamoja nao wazikaliao, mimi ndimi ninayezishikiza nguzo zake.

5*Niliwaambia wenye majivuno: Msijivune! Msielekeze mabaragumu juu, ninyi msionicha!

6Mabaragumu yenu msiyaelekeze juu kabisa, wala msinyoshe shingo mtakaposema!

7Kwani maawioni siko, wala machweoni siko, wala nyikani siko, ukuu utokako.

8Kwani Mungu ndiye anayeamua; yeye ndiye anayenyenyekeza, tena ndiye anayekweza.*1 Sam. 2:7.

9Kwani mkononi mwake Bwana kimo kikombe kilichojaa mvinyo zichemkazo kwa viungo vikali, wote pia wasiomcha Mungu katika nchi huwagawia, wanywe, mpaka wafyonze mashimbi nayo.Sh. 60:5; Yer. 25:15-16.

10Lakini mimi nitamtangaza kale na kale, Mungu wake Yakobo nitamwimbia sifa.

11Nayo mabaragumu yao wasiomcha Mungu nitayavunja yote, lakini mabaragumu yao wamchao yataelekezwa juu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help