2 Mose 32 - Swahili Roehl Bible 1937

Tambiko la ndama ya dhahabu(Taz. 5 Mose 9:8-21.)

1Watu walipoona, ya kuwa Mose anakawia kushuka mlimani, watu wakamkusanyikia Haroni, wakamwambia: Haya! Tufanyie miungu itakayotuongoza! Kwani hatuyajui yaliyompata huyo Mose aliyetutoa katika nchi ya Misri.

2Haroni akawaambia: Ziondoeni pete za dhahabu masikioni kwa wake zenu na kwa wana wenu wa kiume na wa kike, mniletee!

3Ndipo, watu wote walipoziondoa pete za dhahabu za masikioni kwao, wakampelekea Haroni.

4Akazichukua mikononi mwao, akazivunjavunja kwa patasi, akaziyeyusha, akazitengeneza kuwa ndama. Ndipo, waliposema: Huyu ndiye Mungu wako, Isiraeli, aliyekutoa katika nchi ya Misri.

7Lakini Bwana akamwambia Mose: Nenda kushuka! Kwani wao walio ukoo wako, uliowatoa katika nchi ya Misri, wamefanya mabaya

8Wakiondoka upesi katika njia, niliyowaagiza; wamejitengenezea ndama kwa kuyeyusha dhahabu, wakaiangukia na kuitambikia wakisema: Huyu ndiye Mungu wako, Isiraeli, aliyekutoa katika nchi ya Misri.Mose anawaombea Waisiraeli.

30Ikawa kesho yake, ndipo, Mose alipowaambia watu: Ninyi mmekosa kosa kubwa; sasa nitapanda kwenda kwa Bwana, nitazame, kama nitaweza kuwapatia upozi kwa ajili ya kosa lenu.

31Mose aliporudi kwa Bwana akamwambia: Watu wa ukoo huu wamekosa kosa kubwa wakijifanyizia mungu wa dhahabu.Sh. 69:29; Dan. 12:1; Luk. 10:20; Rom. 9:3.

32Lakini sasa uwaondolee kosa lao! Kama haiwezekani, lifute jina langu katika Kitabu chako, ulichokiandika!

33Naye Bwana akamwambia Mose: Anikoseaye ndiye, nitakayemfuta katika Kitabu changu.

34Sasa nenda, uwapeleke watu hawa hapo, nilipokuambia! Naye malaika wangu utamwona, akikutangulia. Lakini siku yangu ya mapatilizo itakapofika, nitawapatilizia hili kosa lao.

35Ndivyo, Bwana alivyowapiga watu wa huo ukoo kwa kuifanya hiyo ndama, Haroni aliyoifanya.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help