2 Samweli 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Dawidi anamwua mpasha habari za kufa kwake Sauli.

1Ikawa, Sauli alipokwisha kufa, Dawidi akarudi kwa kuwapiga Waamaleki; kisha Dawidi akakaa Siklagi siku mbili.

2Ilipokuwa siku ya tatu, mara akaja mtu aliyetoka makambini kwa Sauli, nguo zake zilikuwa zimeraruliwa, napo kichwani pake palikuwa na vumbi; naye alipofika kwake Dawidi akajitupa chini na kumwangukia.

3Dawidi alipomwuliza: Unatoka wapi? akamwambia: Nimekimbia makambini kwa Waisiraeli.

4Ndipo, Dawidi alipomwambia: Nisimulie yaliyofanyika huko! Akamwambia, ya kuwa watu walikimbia penye mapigano, kwa maana wengi wa kwao waliangushwa, wakafa, naye Sauli na mwanawe Yonatani wamekufa.

5Dawidi akamwuliza huyo kijana aliyempasha habari hizi: Umejuaje, ya kuwa Sauli amekufa na mwanawe Yonatani?

6Yule kijana aliyempasha hizi habari akamwambia: Ikanitukia, nifike mlimani kwa Gilboa, mara nikamwona Sauli, akiuegemea mkuki wake, nayo magari pamoja na wapanda farasi wakamsonga.Dawidi anamwombolezea Sauli na Yonatani.

17Kisha Dawidi akatunga ombolezo hili la kumwombolezea Sauli na mwanawe Yonatani.

18Akaagiza kuwafundisha wana wa Yuda wimbo huu wa upindi, nao utaukuta, umeandikwa katika kitabu cha Mnyofu:

19Isiraeli, waliokuwa pambo lake wameuawa vilimani kwako!

Imekuwaje, wakiangushwa hao mafundi wa vita?

20Msiyasimulie Gati, wala msiyatangaze njiani kwa

Askaloni, wasipate kufurahi wanawake wa Wafilisti, wasipige

vigelegele wao wanawake wa kimizimu!

21Msione tena umande wala mvua, ninyi milima ya Gilboa,

yasiwe tena kwenu mashamba yenye malimbuko! Kwani ndiko,

zilikoachwa ngao zao hao mafundi wa vita, ngao yake Sauli

naye, kama hakupakwa mafuta.

22Upindi wake Yonatani ulikuwa hauponyi, ijapo wawe

mafundi wa vita wenye unono, uliotaka kuwaua; upanga wake Sauli haukurudi alani, usipokuwa umeua.

23Sauli na Yonatani walipatana kwa kupendana mioyoni,

hawakutengeka walipoishi, wala walipokufa. Walikuwa wepesi

kuliko kozi, walikuwa wenye nguvu kuliko simba.

24Ninyi wanawake wa Kiisiraeli, mwombolezeeni Sauli!

Kwani aliwavika mavazi ya kifalme yenye urembo mwingi, kisha

hizo nguo zenu akazipamba kwa mapambo ya dhahabu.

25Imekuwaje, wakiangushwa vitani hao mafundi wa vita?

Yonatani akiuawa vilimani kwako?

26Moyo wangu umesongeka kwa ajili yako, maana wewe

ulinipendeza sana, ndugu yangu Yonatani, upendo wako

ulinifurahisha kuliko upendo wa wanawake.

27Imekuwaje, wakiangushwa hao mafundi wa vita? hayo mata

makali ya kupigia vita yakiangamia hivyo?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help