1Nampenda Bwana, kwa kuwa husikia, huisikia sauti yangu, nikimlalamikia.
2Kwa kuwa hunitegea nami sikio lake, kwa hiyo nitamwitia siku zangu zote.
3Matanzi ya kifo yalikuwa yameninasa, masongano ya kuzimu yakanipata, kwa kuona masikitiko nikasongeka.
12Nitawezaje kumrudishia Bwana mema yote, aliyonitendea?
13Nitakiinua kinyweo chenye wokovu, kisha nitalitambikia Jina lake Bwana.
15Ni jambo kuu machoni pa Bwana, wamchao wakifa.Sh. 72:14.
16Mimi nakuomba, Bwana, mimi mtumishi wako, mimi mtumishi wako ni mwana wa mjakazi wako, nawe umenifungulia mafungo yangu.
17Nitakutolea wewe vipaji vya tambiko vya kukushukuru, kisha nitalitambikia Jina lake Bwana.
18Nitamlipa Bwana, niliyomwapia, wote walio ukoo wake wavione na macho yao,
19katika nyua zake Nyumba ya Bwana, katikati mjini mwako, wewe Yerusalemu. Haleluya!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.