Nehemia 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Nehemia anawasaidia wakosao mali.

1Kukawa na kilio kikubwa cha watu na cha wake zao kwa ajili ya ndugu zao Wayuda.

2Wakawako waliosema: Sisi wana wetu wa kiume na wa kike ni wengi, sharti tupate ngano, tule, tusife.

3Walikuwako nao wengine waliosema: Mashamba yetu na mizabibu yetu na nyumba zetu hatuna budi kuzitoa kuwa rehani, tupate ngano katika njaa hii.

4Tena walikuwako wengine waliosema: Tumeyatoa mashamba yetu na mizabibu yetu tulipokopa fedha za kulipa kodi ya mfalme.

5Sasa miili yetu si sawa na miili yao ndugu zetu? Nao wana wetu si sawa na wana wao? Tena inakuwaje, tusipokuwa na budi sisi kuwashurutisha wana wetu wa kiume na wa kike kuwa watumwa? Kweli wako wana wetu wa kike waliouzwa utumwani, namo mikononi mwetu hamna cho chote, kwani mashamba yetu na mizabibu yetu ni ya wengine.

6Makali yangu yakawaka moto, nilipokisikia hicho kilio chao na maneno hayo.

7Nikapiga shauri moyoni, nikawagombeza wakuu wa miji na watawalaji nikiwaambia: Ninyi mnawachuuzia vibaya, kila mtu na ndugu yake. Nikawakusanya kuwa mkutano mkubwa na kuteteana nao,

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help