Luka 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba.

1Ikawa alipokuwa mahali akiomba, akiisha, mwanafunzi wake mmoja akamwambia: Bwana, tufundishe hata sisi kuomba, kama naye Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake!

(2-4: Mat. 6:9-13.)

2Akawaambia: Mnapoomba semeni: Baba yetu ulioko mbinguni, Jina lako litakaswe! Ufalme wako uje! Uyatakayo yatimizwe nchini, kama yanavyotimizwa mbinguni!

3Tupe kila siku chakula chetu cha kututunza!

4Tuondolee makosa yetu! Kwani nasi wenyewe humwondolea kila aliyetukosea. Usituingize majaribuni! Ila tuokoe maovuni!

5*Akawaambia: Kulikuwa na mtu mwenye rafiki; huyu akamwendea usiku wa manane na kumwambia: Rafiki yangu, unikopeshe mikate mitatu!

6Kwani rafiki yangu aliyechwelewa njiani amenifikia, nami sina cha kumwandalia.

7Basi, kwenu yule wa ndani atamjibu nini? Atamwambia: Usinisumbue! Kwani mlango umekwisha fungwa, nao watoto wangu wako kitandani pamoja nami; siwezi kuinuka, nikupe?

8Nawaambiani: Ijapo, asiinuke, ampe, kwa sababu ni rafiki yake, lakini atainuka, ampe yote yampasayo ya mgeni, kwa sababu hana soni ya kuomba.(9-13: Mat. 7:7-11.)

9Nami nawaambiani: Ombeni! ndipo, mtakapopewa. Tafuteni! ndipo, mtakapoona. Pigeni hodi! ndipo, mtakapofunguliwa mlango.

10Kwani kila anayeomba hupewa, naye anayetafuta huona, naye anayepiga hodi hufunguliwa mlango.

11Tena kwenu yuko baba, mwanawe anapomwomba samaki, ampe nyoka, asimpe samaki?

12Au anapomwomba yai, ampe nge?

13Basi, ninyi mlio wabaya mkijua kuwapa watoto wenu vipaji vyema, Baba alioko mbinguni asizidi kuwapa Roho Mtakatifu wanaomwomba?*

Belzebuli.(14-26: Mat. 12:22-30; 43-45; Mar. 3:22-27.)

14*Akawa akifukuza pepo aliyekuwa bubu; naye pepo alipotoka, bubu akaanza kusema. Ndipo, makundi ya watu walipostaajabu.

15Lakini walikuwako waliosema: Nguvu ya Belzebuli, mkuu wa pepo, ndiyo, anayofukuzia pepo.

16Wengine wakamjaribu wakitaka, afanye kielekezo kitokacho mbinguni.

27Ikawa, alipoyasema haya, mwanamke aliyekuwako katika kundi la watu akapaza sauti akimwambia: Lenye shangwe ni tumbo lililokuzaa na maziwa, uliyoyanyonya.Kielekezo cha Yona.(29-32: Mat. 12:38-42.)

29Makundi ya watu walipomkusanyikia, akaanza kusema: Ukoo huu ni ukoo mbaya; wanatafuta kielekezo, lakini hawatapata kielekezo, ila kielekezo cha Yona.(34-36: Mat. 6:22-23.)

34Taa ya mwili ni jicho lako. Basi, jicho lako liking'aa, nao mwili wako wote unao mwanga. Lakini likiwa bovu, nao mwili wako unayo giza.

35Kwa hiyo angalia, mwanga uliomo ndani yako usiwe giza!

36Mwili wako unapokuwa wote unao mwanga, pasiwe upande wenye giza, ndipo, utakapokuwa na mwanga pia, utakuwa kama taa inayokumulikia mwanga wa umeme.

Kuwatisha Mafariseo.

37Alipokuwa katika kusema, Fariseo akamwalika chakulani. Naye akaingia, akakaa mezani.(39-52: Mat. 23:1-36.)

39Bwana akamwambia: Ninyi Mafariseo, vinyweo na vyano mnaviosha nje, lakini ndani ninyi mmejaa mapokonyo na mabaya.

40M wajinga, aliyevifanya vya nje hakuvifanya vya ndani navyo?

41Basi, vile vilivyomo ndani vigawieni watu! Mara vyenu vyote huwa safi.

42Yatawapata, ninyi Mafariseo, kwani fungu la kumi mnalitolea hata mchicha na nyanya na mboga zo zote. Lakini penye hukumu napo penye upendo wa Mungu mnapapita. Haya yawapasa kuyashika pasipo kuyaacha yale.

43Yatawapata, ninyi Mafariseo, kwani nyumbani mwa kuombea mnapenda viti vya mbele, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help