1Bwana akamwambia Mose kwamba:
2Waambie wana wa Isiraeli: Mtu ye yote, kama ni mwana wa Isiraeli au kama ni mgeni akaaye ugenini kwao Waisiraeli atakayetoa hata mmoja tu miongoni mwao walio wa uzao wake na kumpa Moloki sharti auawe, watu wa nchi hiyo sharti wamtupie mawe.
3Nami nitamkazia macho mtu aliye hivyo, nimng'oe katikati yao walio ukoo wake, kwani miongoni mwao walio wa uzao wake ametoa mtu wa kumpa Moloki, kusudi apapatie Patakatifu pangu uchafu, alibezeshe nalo Jina langu takatifu.
4Ijapo watu wa nchi hiyo wayapofushe macho yao, wakiyaona, mtu yule aliyoyafanya alipotoa mtu miongoni mwao walio wa uzao wake na kumpa Moloki, wasipate kumwua,
5mimi na nimkazie macho yangu mtu aliye hivyo nao walio wa kizazi chake, nimng'oe yeye pamoja nao wote waliomfuata na kuufanya ugoni wake wa kumfuata Moloki kufanya ugoni naye, basi, na niwang'oe, watoweke katikati yao walio ukoo wao.
6Hata mtu akiwageukia waganga wa kutiisha mizimu na waaguaji, kufanya ugoni nao, na nimkazie macho yangu aliye hivyo, na nimg'oe katikati yao walio ukoo wake.
7Kwa hiyo jitakaseni, mpate kuwa watakatifu! Kwani mimi Bwana ni Mungu wenu.
9Mtu ye yote atakayemwapiza baba yake au mama yake sharti auawe kabisa; akimwapiza baba yake au mama yake atakuwa amekora manza za kumwagwa damu yake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.