1Siku tano zilipopita, mtambikaji mkuu Anania akatelemka pamoja nao wazee wengine na msemaji aliyitwa Tertulo, wakamsuta Paulo mbele ya mtawala nchi.
2Yule alipoitwa, Tertulo akaanza kumsuta akisema: Kwa nguvu yako, bwana Feliki, tunapata kutengemana sana; na kwa utunzaji wako wewe hili taifa letu limetengenezewa mambo mazuri mengi.
3Hayo yote twayapokea na kukushukuru sana kila siku na kila mahali.
4Lakini nisikuchokeshe kwa maneno mengi; nakuomba utusikilize kidogo kwa utu wako.
5Kwani tumemwona mtu huyu kuwa mwangamizi, akiwaletea kondo Wayuda wote waliopo ulimwenguni po pote, tena ni mkubwa wa chama cha Wanasareti.
22Feliki alipoyasikia haya akawakawilisha, kwani alipata kuelewa na mambo ya njia hiyo. Kwa hiyo akasema: Mkuu wa kikosi Lisia atakapotelemka, nitayatambulisha naye mambo yenu.Tume. 23:26.
23Akamwagiza bwana askari, Paulo alindwe, lakini asifungwe, wala asiwazuie wenziwe kumtumikia au kumjia.Tume. 27:3.
24Siku zilipopita, Feliki akaja pamoja na mkewe Dirusila aliyekuwa Myuda, akatuma kumwita Paulo, akamsikiliza, akimwonyesha, kumtegemea Kristo Yesu kulivyo.
25Lakini alipoeleza mambo ya kupata wongofu na ya kuziepuka tamaa na ya hukumu itakayokuwapo, Feliki akaingiwa na woga, akajibu: Sasa hivi jiendee tu!
26Hapo, nitakapopata mapumziko, nitakuita tena. Vile vile alingojea kupenyezewa fedha na Paulo, amfungue. Kwa hiyo akamwita mara kwa mara, aongee naye.
27Lakini miaka miwili ilipopita, Porkio Festo akampokea Feliki kazi yake. Feliki akataka kuwapendelea Wayuda, kwa hiyo akamwacha Paulo kifungoni.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.