Marko 16 - Swahili Roehl Bible 1937

Kufufuka.(1-8: Mat. 28:1-8; Luk. 24:1-12; Yoh. 20:1-10.)

1*Siku ya mapumziko ilipokwisha pita, ndipo, Maria Magadalene na Maria, mama yake Yakobo, na Salome waliponunua manukato, wapate kwenda kumpaka.

2Siku ya kwanza ya juma asubuhi na mapema wakajidamka, wakaenda kaburini, jua lilipochomoza.

3Wakasema wao kwa wao: Nani atatufingirishia lile jiwe, litoke mlangoni pa kaburi?

4Walipotazama wakaona, jiwe limekwisha fingirishwa; kwani lilikuwa kubwa mno.

5Walipoingia kaburini wakaona kijana, amekaa kuumeni, amejitanda nguo nyeupe, wakaingiwa na kituko.

6Naye akawaambia: Msistuke! Mnamtafuta Yesu wa Nasareti aliyewambwa msalabani, amefufuliwa, hayumo humu. Patazameni mahali, walipomweka!

7Lakini nendeni, mwaambie wanafunzi wake na Petero, ya kuwa anawatangulia ninyi kwenda Galilea! Huko ndiko, mtakakomwona, kama alivyowaambia.Kupaa mbinguni.(19: Luk. 24:50-53; Tume. 1:4-11.)

19Bwana Yesu alipokwisha kusema nao akachukuliwa na kupazwa mbinguni, akaketi kuumeni kwa Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help