Yohana 19 - Swahili Roehl Bible 1937

Kilemba cha miiba.

1Ndipo, Pilato alipomchukua Yesu, akampiga viboko.

2Kisha askari wakasuka kilemba cha miiba, wakamvika kichwani, wakamvika hata nguo ya kifalme,

3wakamjia wakisema: Pongezi, mfalme wa Wayuda! wakampiga makofi.

4Pilato alipotoka tena nje, akawaambia: Tazameni, ninampeleka kwenu nje, mpate kutambua, ya kuwa sioni kwake neno la kumhukumu.

5Yesu akatoka nje, amekivaa kilemba cha miiba na nguo ya kifalme. Pilato akawaambia: Mtazameni mtu huyu!

6Watambikaji wakuu na watumishi walipomwona wakapiga makelele wakisema: Mwambe msalabani! Mwambe msalabani! Pilato alipowaambia: Mchukueni ninyi, mmwambe msalabani! Kwani mimi sioni kwake neno la kumhukumu.

7Wayuda wakamjibu: Sisi tuko na Maonyo, kwa Maonyo hayo sharti afe, kwani amejifanya kuwa Mwana wa Mungu.(6-30: Mat. 27:31-50; Mar. 15:20-37; Luk. 23:26-46.)

16Basi, hapo ndipo, alipomtoa, awambwe msalabani.

I.N.R.I.

Wakampeleka Yesu;

17naye akajichukulia mwenyewe msalaba wake alipotoka kwenda mahali panapoitwa Fuvu la Kichwa, jina lake Kiebureo: Golgota.

18Ndipo, walipomwamba msalabani; tena pamoja naye wakawamba misalabani wengine wawili, huku na huko, lakini Yesu katikati.

19Pilato akaandika mwandiko, akaubandika msalabani juu; hapo palikuwa pameandikwa: YESU WA NASARETI, MFALME WA WAYUDA.

20Mwandiko huo Wayuda wengi waliusoma, kwani mahali pale, Yesu alipowambwa msalabani, palikuwa karibu na mji. Nao ulikuwa umeandikwa Kiebureo na Kiroma na Kigriki.

21Watambikaji wakuu wa Wayuda walipomwambia Pilato: Usiandike: Mfalme wa Wayuda, ila: Huyu amesema: Mimi ni mfalme wa Wayuda!

22Pilato akajibu: Niliyoyaandika, basi, nimekwisha kuyaandika.

Nguo za Yesu.

23Askari walipokwisha kumwamba Yesu msalabani wakayachukua mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kila askari fungu moja, wakaichukua hata kanzu. Lakini ile kanzu ilikuwa pasipo mshono, toka juu yote ilikuwa imefumwa tu.

24Kwa hiyo wakaambiana: Tusiipasue, ila tuipigie kura, ajulike atakayeipata. Imekuwa hivyo, litimie lililoandikwa:

Wakajigawanyia nguo zangu,

nalo vazi langu zuri wakalipigia kura.

Ndio askari waliofanya hivyo.Yohana na Maria.

25Lakini penye msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama akina mama yake na ndugu ya mama yake, jina lake Maria wa Klofa, na Maria Magadalene.

26Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi, aliyempenda, akisimama karibu, akamwambia mama yake: Mama, tazama, mwana wako huyu!Kumzika Yesu.(38-42: Mat. 27:57-61; Mar. 15:42-47; Luk. 23:50-55.)

38Hayo yalipokwisha, akatokea Yosefu wa Arimatia aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini alikuwa amejifichaficha kwa kuwaogopa Wayuda; yeye ndiye aliyemwomba Pilato ruhusa ya kuuondoa mwili wa Yesu. Pilato alipompa ruhusa, akaenda, akauondoa mwili wake.

39Pakaja Nikodemo naye, ni yule aliyemjia usiku hapo kwanza, akaleta manemane iliyochanganyika na uvumba, yapata kama mizigo miwili.Yoh. 3:2; Mat. 2:11.

40Kisha wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga kwa sanda pamoja na yale manukato, kama Wayuda walivyozoea kuzika.

41Mahali pale, alipowambwa msalabani palikuwa na kiunga, namo mle kiungani mlikuwa na kaburi jipya, ambalo hajazikwa mtu bado ndani yake.

42Kwa sababu ni siku ya kuandalia kwa Wayuda, wakamweka Yesu mle, kwani lile kaburi lilikuwa karibu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help