1Bwana akaniambia: Jitwalie ubao mkubwa, kauandike kwa kalamu ya kimtu, watu waweze kuusoma: Teka upesi! Pokonya hima!
2Nami nitachukua mashahidi welekevu, wanishuhudie, ni mtambikaji Uria na Zakaria, mwana wa Yeberekia.
3Kisha nikafika kwake mfumbuaji wa kike; akapata mimba, akazaa mwana wa kiume. Bwana akaniambia: Ita jina lake Teka upesi! Pokonya hima!
4Kwani kijana atakapokuwa hajajua kuita: Baba! au: Mama! watu watakuwa wameyachukua mapato ya Damasko na mateka ya Samaria, wakiyapeleka machoni pake mfalme wa Asuri.
5Bwana akasema tena na mimi mara nyingine akiniambia:
9Kasirikeni, ninyi makabila ya watu, kalegeeni kwa kituko! Sikilizeni, nyote mkaao katika nchi za mbali! Jifungeni, kisha legeeni kwa kituko!Watu sharti wamtegemee Mungu tu.
11Kwani hivi ndivyo, Bwana alivyoniambia aliponishika mkono na kunionya, nisiifuate njia ya watu wa ukoo huu, akisema:
12Msiite angamizo vyote, watu wa ukoo huu wanavyoviita angamizo! Wala msiyaogope, wanayoyaogopa, wala msiyastukie!
13Ila mtakaseni Bwana Mwenye vikosi! Yeye ndiye, mmwogope na kumstukia!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.