1Akanirudisha penye kuiingilia Nyumba hii, mara nikaona maji yaliyotoka chini ya kizingiti cha Nyumba hii kwenda upande wa maawioni kwa jua, kwani upande wa mbele wa Nyumba hii ulielekea maawioni kwa jua; nayo hayo maji yakachuruzika chini ya upande wa kuumeni wa Nyumba hii, kusini penye meza ya kutambikia.Mipaka ya nchi.
13Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Huu ndio mpaka wa nchi hiyo, mtakayojigawanyia kuwa mafungu yao yale mashina kumi na mawili ya Isiraeli, Yosefu tu apate mafungu mawili.1 Mose 48:5; Yos. 17:17.
14Mtajigawanyia mafungu yaliyo sawasawa kwa kila mtu na ndugu yake, yawe yenu, kwa kuwa niliapa na kuuinua mkono wangu ya kwamba: Nitawapa baba zenu; kwa hiyo nchi hii itawaangukia kuwa mafungu yenu.
15Nao huu ndio mpaka wa nchi hiyo: upande wa kaskazini toka kwenye Bahari Kubwa unakwenda Hetiloni kufika Sedadi,4 Mose 34:2-12.
16Hamati, Berota, Siburemu ulioko katikati ya mpaka wa Damasko na mpaka wa Hamati na Haseri wa kati ulioko kwenye mpaka wa Haurani.
17Ndivyo, mpaka utakavyotoka baharini kwenda mpaka Hasari-Enoni, mpaka wa Damasko uwe upande wa kaskazini, nao mpaka wa Hamati ukae kaskazini. Huu ndio mpaka wa kaskazini.
18Nao mpaka wa maawioni kwa jua uufuate mto wa Yordani toka Damasko na Haurani, tena toka Gileadi na nchi ya Isiraeli; huu mpaka mwupime toka hapo hata bahari ya maawioni kwa jua, uwe mpaka wa maawioni kwa jua.
19Nao upande wa kusini uelekeao kwenye jua kali uanzie Tamari kwenda Kadesi kwenye Maji ya Magomvi, kisha ufuate ule mto unaoingia katika Bahari Kubwa; huu ndio mpaka wa kusini uelekeao kwenye jua kali.4 Mose 20:13; 34:5.
20Nao upande wa baharini mpaka ni Bahari Kubwa toka hapo kufika ng'ambo ya Hamati; huu ndio mpaka wa upande wa baharini.
21Nchi mtajigawanyia kwa mashina ya Isiraeli.
22Hapo, mtakapoipigia kura za kujipatia mafungu yatakayokuwa yenu, sharti mwapatie nao wageni wakaao kwenu katikati waliozaa wana katikati yenu. Nao watakuwa kwenu kama wazalia waliomo miongoni mwa wana wa Isiraeli; kwa hiyo sharti wapigiwe kura pamoja nanyi za kujipatia mafungu yatakayokuwa yao katikati ya mashina ya Waisiraeli.2 Mose 22:21.
23Kwa shina lilelile, mgeni atakakokaa, ndiko, mtakakompa fungu, liwe lake. Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.