1Ikiwa hivyo, Wayuda wanapitaje wengine? Au kutahiriwa kunafaaje?
2Hufaa sana hapo na hapo. Kwanza waliagiziwa maneno yake Mungu.
5Lakini upotovu wetu ukiutokeza wongofu wake Mungu, tutasemaje? Je? Mungu naye siye mpotovu akitutolea makali? (Nasema kimtu.)
6La, sivyo! Mungu angaliwezaje kuuhukumu ulimwengu?
7Lakini kweli ya Mungu ikiongezwa utukufu na uwongo wangu, mimi tena ninahukumiwaje kama mkosaji?
8Hivyo sivyo, tunavyosingiziwa, wengine wakitusema sisi, kwamba tumesema: Na tuyafanye yaliyo maovu, yaliyo mema yapate kutokea? Hao hukumu yao inapasa kabisa.
9Sasa Je? Tumewapita? Hapana, hata kidogo tu. Kwani hapo mbele tumewasuta wote, Wayuda na Wagriki, kwamba: Wote ni wakosaji,
11Hakuna aliye mwenye akili, hakuna anayemtafuta Mungu.
12Wote pamoja wamepotelewa na njia, wote ni waovu.
Hakuna anayefanya mema, hakuna hata mmoja.
13Makoo yao huwa makaburi yaliyo wazi,
ndimi zao huzitumia uwongo tu,
sumu ya pili imo midomoni mwao.
14Vinywa vyao hujaa matusi na uchungu,
15miguu yao hupiga mbio kuja kumwaga damu.
16Maangamizo na mavunjiko huzijulisha njia zao,
17lakini njia ya utengemenao hawaijui.
18Kumwogopa Mungu hakupo machoni pao.Wongofu wa Kimungu.
21*Lakini sasa wongofu wa Kimungu umefunuliwa pasipo Maonyo; nao unashuhudiwa na Maonyo pamoja na Wafumbuaji kwamba:
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.