1*Watoza kodi na wakosaji wo wote walipokuwa wanamjia, wamsikilize,
2Mafariseo na waandishi wakanung'unika wakisema: Huyu huwapokea wakosaji, ale pamoja nao.Mwana mpotevu.
11*Kisha akasema: Kulikuwa na mtu mwenye wana wawili.
12Aliye mdogo wao akamwambia baba yake: Baba, nipe fungu la mali litakalokuwa langu! Ndipo, alipowagawanyia mali.
13Siku chache zilipopita, mwana mdogo akavikusanya vyote, akajiendea kufika katika nchi ya mbali. Huko akazitapanya mali zake kwa kuzitumia ovyoovyo tu.
25Lakini mwana wake mkubwa alikuwa shambani; alipokuja na kufika karibu ya mjini akasikia nyimbo na michezo.
26Akaita mtumwa mmoja, akamwuliza: Mambo hayo ya nini?
27Naye akamwambia: Ndugu yako amekuja; ndipo, baba yako alipomchinjia yule ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yuko mzima.
28Akakasirika sana, hakutaka kuingia. Lakini baba yake alipotoka na kumbembeleza,Luk. 15:2.
29akamjibu baba yake akimwambia: Tazama, miaka hii yote ninakutumikia; tena hakuna agizo lako, nisilolifanya. Nawe hujanipa hata kibuzi, nipate kushangilia na rafiki zangu.
30Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyekula mali zako pamoja na wagoni, umemchinjia yule ndama aliyenona.
31Naye akamwambia: Mwanangu, wewe siku zote uko pamoja nami, nayo yote, niliyo nayo, ni yako.
32Lakini imetupasa kushangilia na kufurahi, kwani huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka. Alikuwa amepotea, naye ameonekana tena.*
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.