Luka 2 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuzaliwa kwake Yesu.

1*Ikawa siku zile, amri ikitoka kwa Kaisari Augusto, walimwengu wote waandikiwe kodi;

2huko kuandikwa kulikuwa kwa kwanza, kukawa siku zile, Kirenio alipotawala Ushami.

3Ndipo, watu wote waliposhika njia za kwenda kuandikiwa kodi, kila mtu akaenda mjini kwao.

4Yosefu naye akaondoka Galilea katika mji wa Nasareti kwenda Yudea katika mji wa Dawidi unaoitwa Beti-Lehemu, kwa kuwa yeye alikuwa wa mlango na wa udugu wa Dawidi.

5Akaenda pamoja na mkewe Maria aliyeposwa naye, waandikiwe kodi; naye alikuwa ana mimba.

8Kulikuwa na wachungaji katika nchi ileile, walilala malishoni na kulilinda kundi lao kwa zamu ya usiku.

9Ndiko, malaika wa Bwana alikowatokea, nao utukufu wa Bwana ukawamulikia po pote, wakashikwa na woga mwingi.

10Lakini malaika akawaambia: Msiogope! kwani tazameni, ninawapigia mbiu njema yenye furaha kuu itakayowajia watu wote.

11Kwani mmezaliwa leo mwokozi wenu katika mji wa Dawidi, ndiye Bwana Kristo.

12Nacho kielekezo chenu ni hiki: mtaona kitoto kichanga, kimevikwa nguo za kitoto, kimelazwa waliamo ng'ombe.

13Mara wakawa pamoja na yule malaika wingi wa vikosi vya mbinguni, wakamsifu Mungu wakiimba:

14Utukufu ni wa Mungu mbinguni juu,

nchini uko utengemani kwa watu wampendezao.

15*Ikawa, malaika walipoondoka kwao kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezana wao kwa wao: Haya! Twende, tufike hata Beti-Lehemu, tulitazame jambo hilo lililokuwapo, Bwana alilotutambulisha!

16Wakaenda mbio, wakawakuta, akina Maria na Yosefu na kitoto kichanga, kimelazwa waliamo ng'ombe.

17Walipokwisha kumwona wakalitambulisha lile neno, waliloambiwa na kitoto hiki.Simeoni.

22*Siku zao zilipotimia za weuo, aliouagiza Mose, wakampeleka Yerusalemu, wamtokeze kwake Bwana.

25*Huko Yerusalemu kulikuwa na mtu, jina lake Simeoni. Mtu huyo alikuwa mwongofu mwenye kumcha Mungu, akaungoja utulivu wa Isiraeli; nayo Roho takatifu ilikuwa naye.

33Baba yake na mama yake walipokuwa wakiyastaajabu aliyosemewa,Yesu mwenye miaka 12 Nyumbani mwa Mungu.

41*Wazazi wake huenda Yerusalemu kila mwaka kula sikukuu ya Pasaka.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help