1Mfalme Salomo akawa mfalme wa Waisiraeli wote;Nguvu za Salomo.
21Salomo akawa akizitawala nchi za kifalme zote kutoka lile jito kubwa kuifikia nchi ya Wafilisti hata mipaka ya Misri; walimletea mahongo, wakamtumikia Salomo siku zake zote za kuwapo.
22Vyakula, Salomo alivyovitumia kwa siku moja, vilikuwa kori 30, ndio frasila 300 za unga mzuri na kori 60, ndio frasila 600 za unga mwingine;
23tena ng'ombe 10 waliononeshwa na ng'ombe 20 wa malishoni na kondoo 100, tena kulungu na paa na funo na mabata waliononeshwa hawakuhesabiwa.
24Kwani alikuwa akizitawala nchi zote za ng'ambo ya huku ya lile jito kutoka Tifusa hata Gaza, nao wafalme wote wa ng'ambo ya huku ya lile jito aliwatawala, kukawa na utengemano katika nchi zake zote zilizomzunguka.
25Wayuda na Waisiraeli wakakaa na kutulia kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mkuyu wake kutoka Dani kufikia Beri-Seba siku zote, Salomo alizokuwapo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.