1*Sasa hakuna tena kinachowapatiliza walio katika Kristo Yesu, wasioendelea kimtu, ila Kiroho.Utukufu tutakaofunuliwa.
18*Kwani naona, ya kuwa mateso ya siku hizi za sasa si kitu, tukiyafananisha na ule utukufu, tutakaofunuliwa sisi.
24*Kwani kingojeo, ambacho tuliokolewa, tuwe nacho, hicho ndicho; lakini kingojeo kinachoonekana machoni sicho kingojeo. kwani hilo, mtu analoliona, analingojeaje?
33*Yuko nani atakayewasuta waliochaguliwa na Mungu? Mungu yuko anayewashuhudia kuwa waongofu.
34Yuko nani atakayewahukumu? Kristo Yesu yuko aliyekufa kwa ajili yao, na kupita hapo amefufuka, yuko kuumeni kwa Mungu na kutusemea sisi.Rom. 8:1; 1 Yoh. 2:1.
35Yuko nani atakayetutenga na upendo wake Kristo? Maumivu au masongano au mafukuzo au njaa au uchi au maponzo au panga?
36Ndivyo vilivyoandikwa kwamba:
Kumbe ni kwa ajili yako wewe, tukiuawa kila siku
tukihesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa tu!Sh. 44:23; 1 Kor. 4:9; 2 Kor. 4:11.
37Lakini katika mambo hayo yote tunazidi kushinda kabisa kwa nguvu yake yeye aliyetupenda sisi.Yoh. 16:33; Ufu. 12:11.
38Kwani hili nimelitambua kuwa kweli kabisa: Kukiwa kufa au kuishi, wakiwa malaika au wenye nguvu, yakiwa ya leo au ya kale, zikiwa nguvuEf. 6:12.
39za mbinguni juu au za kuzimuni chini, vikiwa viumbe vyo vyote vingine, hakuna kitakachoweza kututenga sisi na upendo wake Mungu uliotutokea katika Kristo Yesu, Bwana wetu.*
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.