1Baada ya mambo hayo, makali ya mfalme Ahaswerosi yalipotulia, akamkumbuka Wasti nayo, aliyoyafanya, nalo shauri, alilokatiwa.
2Ndipo, vijana wa mfalme waliomtumikia waliposema: Watu na wamtafutie mfalme vijana wa kike, walio wanawali wenye sura nzuri!
3Mfalme na aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, wawakusanye vijana wa kike wote walio wanawali wenye sura nzuri, wawapeleke Susani jumbani mwa mfalme na kuwatia chumbani mwa wanawake mkononi mwake Hegai aliye mtumishi wa mfalme wa nyumbani wa kuwaangalia wanawake, kisha wapewe vyombo vyao vya kutengenezea uzuri.
4Naye kijana atakayempendeza mfalme na awe mkewe mfalme mahali pa wasti. Neno hili likampendeza mfalme, akafanya hivyo.
5Mle Susani, mlimokuwa wa jumba la mfalme, mlikuwa na mtu wa Kiyuda, jina lake Mordekai, mwana wa Yairi, mwana wa Simei, mwana wa Kisi, wa mlango wa Benyamini.Mordekai anavumbua njama ya kumwua mfalme.
21Siku zile, Mordekai alipokaa langoni pa mfalme, watumishi wawili wa mfalme wa nyumbani waliokuwa walinda mlango, ndio Bigitana na Teresi, wakakasirika sana, wakatafuta njia ya kumwua mfalme Ahaswerosi kwa mikono yao.
22Mordekai akapata kulijua shauri hilo, akamsimulia Esteri, mkewe mfalme, naye Esteri akamwambia mfalme katika jina la Mordekai.
23Kisha shauri hilo likanyatiwa, hata likavumbulikana, nao wale wawili wakatundikwa katika mti. Mambo haya yakaandikwa katika kitabu cha mambo ya siku machoni pa mfalme.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.