Mashangilio 54 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuuomba msaada wa Mungu penye masongano.

1-2Kwa mwimbishaji. Fundisho la Dawidi la kuimbia mazeze; alilitunga hapo, watu wa Zifu walipokwenda kumwambia Sauli: Hujui, ya kuwa Dawidi amejificha kwetu?

3Mungu, kwa ajili ya Jina lako niokoe!

Kwa nguvu zako kuu niamulie!

4Mungu, maombo yangu yasikie na kuyasikiliza maneno ya kinywa changu!

5Kwani wasio wa kwetu wameniinukia, wanaitafuta roho yangu wao wakorofi, lakini yeye aliye Mungu hawamtazami.

6Ninajua: Mungu ndiye anayenisaidia, ndiye anayeishikiza roho yangu.

7Uwarudishie ubaya wao waninyatiao! Kwa maana u mkweli uwamalize!

8Kisha nitakutolea ng'ombe za tambiko kwa kupendezwa, nitalishukuru Jina lako kuwa lenye wema.

9Kwani katika masongano yote umeniopoa, macho yangu yakapata kuwafurahia wachukivu wangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help