Mifano 25 - Swahili Roehl Bible 1937

Macheo ya kweli ni mshahara wa werevu wa kweli.

1Hii nayo ni mifano ya Salomo, waliyoikusanya watu wa Hizikia, mfalme wa Yuda.

2Utukufu wake Mungu ni kufunika jambo,

utukufu wao wafalme ni kufunua jambo.

3Kama mbingu zilivyoko juu, kama nchi ilivyoko nako kuzimuni,

ndivyo, mioyo ya wafalme inavyotushinda, isichunguzike.

4Mtu akiondoa mitapo katika fedha

hutengeneza chombo kinachomfaa mwenye kuyeyusha.

5Mtu akimwondoa asiyemcha Mungu machoni pake mfalme,

kiti chake cha kifalme hupata nguvu kwa wongofu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help