Esteri 10 - Swahili Roehl Bible 1937

Mordekai anazitumia nguvu zake kuwasaidia Wayuda.

1Mfalme Ahaswerosi akatoza kodi katika hiyo nchi, hata katika visiwa vya baharini.

2Matendo yote ya uwezo wake na ya nguvu zake na habari zote za macheo makuu, mfalme aliyompa Mordekai, hayakuandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za wafalme wao Wamedi na Wapersia?Est. 8:2,15.

3Kwani Myuda Mordekai alikuwa wa pili kwake mfalme Ahaswerosi na mkuu kwa Wayuda, akapendwa na ndugu zake waliokuwa wengi, kwa kuwa aliwatakia mema walio ukoo wake, akasema nao wote walio wa kizazi chake maneno ya utengemano.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help