1Manase alikuwa mwenye miaka 12 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 55 mle Yerusalemu.
2Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana kwa kuyafuata matapisho ya wamizimu, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Isiraeli.Manase analijenga boma la Yerusalemu.
14Baada ya hayo akaujenga ukuta wa nje wa mji wa Dawidi ulioko upande wa machweoni kwa jua kulielekea bonde la kijito cha Gihoni mpaka kufika penye lango la Samaki na kuzunguka Ofeli, akaupandisha kwenda juu sana. Tena akaweka wakuu wa vikosi katika miji yote yenye maboma katika nchi ya Yuda.
Manase anaondoa matambiko ya kimizimu.15Kisha akaiondoa miungu migeni pamoja na kile kinyago Nyumbani mwa Bwana, nazo meza zote za kutambikia, alizozijenga milimani penye Nyumba ya Bwana namo Yerusalemu, akazitupa huko nje ya mji.
16Akaitengeneza tena meza ya kumtambikia Bwana, akachoma juu yake ng'ombe za tambiko za kushukuru na za kusifu, nao Wayuda akawaagiza kumtumikia Bwana Mungu wa Isiraeli.
17Lakini watu hawakuacha kutambika vilimani, lakini huko nako siku zile wakamtambikia Bwana Mungu wao tu.
Kufa kwake Manase.18Mambo mengine ya Manase na maombo yake, aliyomwomba Mungu wake, na mambo ya wachunguzaji waliosema naye katika Jina la Bwana Mungu wa Isiraeli tunayaona, yametiwa katika mambo ya wafalme wa Waisiraeli.
19Maombo yake na vilio vyake na makosa yake yote ya kuvunja maagano na mahali, alipojenga vijumba vya kutambikia vilimani, napo aliposimamisha miti ya Ashera na vinyago vingine, alipokuwa hajajinyenyekeza bado, yote yamekwisha kuandikwa katika mambo ya wachunguzaji.
20Kisha Manase akaja kulala na baba zake, wakamzika nyumbani mwake, naye mwanawe Amoni akawa mfalme mahali pake.
Mfalme Amoni anauawa kwa ubaya wake.21Amoni alikuwa mwenye miaka 22 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 2 mle Yerusalemu.
22Akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya, navyo vinyago vyote, baba yake Manase alivyovitengeneza, Amoni akavitambikia na kuvitumikia.
23Hakujinyenyekeza mbele ya Bwana, kama baba yake Manase alivyojinyenyekeza, kwani yeye Amoni alikora manza nyingi.2 Mambo 33:12.
24Ndipo, watumishi wake walipomlia njama, wakamwua nyumbani mwake.
25Lakini watu wa nchi hiyo wakawaua wote waliomlia mfalme Amoni njama, kisha hao watu wa nchi hiyo wakamfanya mwanawe Yosia kuwa mfalme mahali pake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.