1Bwana akamwambia Mose: Nenda, uondoke hapa, wewe na watu hawa, niliowatoa katika nchi ya Misri, uwapeleke katika nchi ile, niliyomwapia Aburahamu na Isaka na Yakobo kwamba: Nchi hii nitawapa wao wa uzao wako.
7Mose akaambiwa, lile Hema alichukue kila mara, alipige nje ya makambi, iwe mbali ya makambi, nalo aliite Hema la Mkutano, kila atakayemtafuta Bwana atoke kwenda kwenye Hema la Mkutano lililoko nje ya makambi.
12Mose akamwambia Bwana: Tazama, wewe unaniambia: Wapeleke watu hawa! Lakini hujanijulisha bado, kama ni nani, utakayemtuma kwenda na mimi; tena ulisema: Ninakujua kwa jina, maana umeona upendeleo machoni pangu.Mose anataka kuuona utukufu wa Bwana.
18Mose akaomba: Nionyeshe utukufu wako!
19Akaitikia kwamba: Nitaupitisha wema wangu wote machoni pako, nalo Jina langu la Bwana nitalitamka kwa sauti kuu masikioni pako. Mimi nitakayemhurumia, nitamhurumia kweli; nitakayemwonea uchungu, nitamwonea uchungu wa kweli.Rom. 9:15.
20Akamwambia tena: Lakini uso wangu huwezi kuuona, kwani hakuna mtu atakayekuwa yu hai akiisha kuniona.1 Mose 32:30; Yes. 6:5; 1 Tim. 6:16.
21Bwana akamwambia tena: Nitakuonyesha mahali, ndipo upate kusimama juu ya mwamba.1 Fal. 19:8-13.
22Hapo, utukufu wangu utakapopita, nitakuweka katika pango la huo mwamba na kukukingia kwa mkono wangu, mpaka nitakapokwisha kupita.2 Mose 34:5-6; 24:11.
23Nitakapouondoa mkono wangu, utaweza kutazama nyuma yangu, lakini uso wangu mtu hawezi kuuona.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.