Waroma 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Mapato ya anguko lao Waisiraeli.

1Basi, niseme: Mungu aliwatupa walio ukoo wake? La, sivyo! Kwani hata mimi ni Mwisiraeli, ni wa uzao wake Aburahamu, ni wa shina la Benyamini.

2Mungu hakuwatupa walio ukoo wake,

aliowatambua kale. Au hamyajui, Maandiko yanayoyasema, Elia alipomlalamikia Mungu kwa ajili ya Waisiraeli?

8Mungu aliwapa roho ya usingizi

na macho yasiyoona na masikio yasiyosikia

mpaka siku hii ya leo.

10Macho yao na yatiwe giza, wasione,

migongo yao nayo ipindike siku zao zote!

11Basi, niseme: Walijikwalia, waanguke tu? La, sivyo! Ila maanguko yao yamewaletea wamizimu wokovu, wenyewe wawaonee wivu, wapate kujikaza.

27Nalo hili ni agano, ninalolifanya nao:

Nitayaondoa makosa yao.

28Kwa hivyo, wanavyoukataa Utume mwema, ndio wachukivu kwa ajili yenu; lakini kwa hivyo, walivyochaguliwa, ndio wapendwa kwa ajili ya baba zao.

29Kwani Mungu hayajutii magawio na wito wake.

30Kama ninyi: Kale mlimkataa Mungu, lakini sasa mmehurumiwa kwa ajili ya ukatavu wao hao;

31vivyo hivyo hata hao sasa wameikataa ile huruma iliyowatokea, kwamba nao siku ziwafikie, watakapohurumiwa.

32Kwani Mungu aliwaunga wote pia, wamkatae, apate kuwahurumia wote.

33*Tazameni, jinsi ujuzi na utambuzi wake Mungu unavyofurika kuwa mwingi! Kweli maamuzi yake hayachunguziki, njia zake nazo hazinyatiliki!Rom. 9:23; 10:12; Yes. 45:15; 55:8-9.

34Kwani yuko nani aliyeyatambua mawazo ya Bwana? Au yuko nani aliyekula njama naye?Iy. 15:8; Yes. 40:13; Yer. 23:18; 1 Kor. 2:16.

35Au yuko nani aliyeanza kumpa kitu, apate kulipwa naye?Iy. 41:3-11.

36Kwani yote yalitoka kwake yeye, yakafanywa naye yeye, tena yatarudi kwake yeye. Yeye ndiye atakayetukuzwa kale na kale. Amin.*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help