2 Mose 19 - Swahili Roehl Bible 1937

Waisiraeli wanafika Sinai.

1Katika mwezi wa tatu tangu hapo, wana wa Isiraeli walipotoka katika nchi ya Misri, siku hiyohiyo wakafika nyikani kwa Sinai.

2Walipoondoka Refidimu, wakafika nyikani kwa Sinai; nao Waisiraeli wlipoyapiga makambi yao wakayapiga ng'ambo ya huku kwenye huo mlima.

3Naye Mose akaupanda huo mlima kwenda kwake Mungu, Bwana alipomwita huko mlimani, akamwambia: Hivi ndivyo, utakavyowaambia wao wa mlango wa Yakobo na kuwatangazia wana wa Isiraeli:

4Ninyi mmeyaona niliyowafanyizia Wamisri, nikawachukua ninyi, kama tai anavyowachukua watoto wake mabawani, nikawafikisha kwangu.Mungu anatokea mlimani kwa Sinai.

16Siku ya tatu ilipofika, ilipokuwa asubuhi, zikasikilika ngurumo, nao umeme ukapiga, nako mlimani juu kukawa na wingu jeusi, nao mlio wa baragumu lenye nguvu ukasikilika, nao watu wote waliokuwa makambini wakatetemeka.Ebr. 12:21.

17Ndipo, Mose alipowatoa watu makambini, waje kukutana na Mungu, wakajipanga mlimani chini.

18Lakini mlima wote wa Sinai ulitoka moshi, kwa kuwa Bwana aliutelemkia kwa moto, nao moshi wake ukapanda, kama moshi wa tanuru, nao mlima wote ukatetemeka sana,

19nao mlio wa lile baragumu ukaendelea, ukazidi sana. Mose akasema, naye Mungu akamwitikia na kupaza sauti.Tume. 7:38.

20Bwana alipokwisha kushuka huko kwenye mlima wa sinai na kufika kileleni juu ya mlima huu, Bwana akamwita Mose kufika kileleni juu ya mlima huu, naye Mose akapanda.

21Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Shuka, uwaonye hawa watu, wasijivunjie njia ya kufika kwa Bwana, wapate kumwona, wasife wengi miongoni mwao.

22Nao watambikaji watakaomkaribia Bwana, sharti wajieue, Bwana asije, akawaponda.

23Lakini Mose akamwambia Bwana: Hawa watu hawawezi kupanda mlimani kwa Sinai, kwani wewe mwenyewe umetuonya na kuniagiza kwamba: Kata mpaka wa mlima huu na kuueua, wasiuguse.

24Ndipo, Bwana alipomwambia: Nenda, ushuke! Kisha upande wewe, naye Haroni pamoja na wewe! Lakini watambikaji na watu wasijivunjie njia ya kupanda kwake Bwana, asije, akawaponda.

25Kisha Mose akatelemka kwenda kwao hao watu, akawaambia maneno hayo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help