Mashangilio 71 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba, Mungu asituache, tutakapokuwa wazee.

1Wewe Bwana, nimekukimbilia, sitapatwa na soni kale na kale.

2Kwa kuwa u mwongofu, niopoe na kuniponya! Nitegee sikio lako, ukaniokoe!

3Niwie mwamba wenye nguvu, niujie siku zote, maana uliniagia, ya kuwa utaniokoa. Kwani mwamba wangu na boma langu ndiwe wewe.

4Mungu wangu, niponye mikononi mwao wasiokucha! Namo mikononi mwao wapotovu namo mwao wakorofi!

5Kwani wewe Bwana Mungu, u kingojeo changu, u kimbilio langu tangu hapo, nilipokuwa mtoto.

6Nimejishikiza kwako tangu hapo, nilipozaliwa, wewe ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu; ninakushangilia siku zote.

7Kwao wengi ni kama kielekezo, wakiniona, nawe ndiwe kimbilio langu lenye nguvu.

16Ninaendelea bado kwa nguvu za Bwana Mungu zilizo kuu, ninayowakumbusha si mengine, ni wongofu wako tu.

17Mungu, ulinifundisha tangu hapo, nilipokuwa mtoto; kwa hiyo ninayatangaza mataajabu yako.1 Sam. 7:12.

18Sasa napo hapo, nitakapokuwa mzee mwenye mvi, usiniache, Mungu, niwatangazie vizazi vingi kazi za mkono wako nayo matendo yako yenye nguvu kwao wote watakaokuwapo.Sh. 71:9; Yes. 46:4.

19Wongofu wako, Mungu, unakua kufika hata mbinguni, wewe ndiwe ufanyaye mambo makuu. Mungu, afananaye na wewe yuko nani?2 Mose 15:11.

20Wewe ulipotuacha, tuliona masongano mengi na mabaya; lakini utaturudisha tena, utupatie uzima, utatutoa huko ndani ya nchi, utuweke juu yake.1 Sam. 2:6.

21Ukuu, utakaonipa, utazidi, utakaponigeukia, unitulize moyo.

22Nami nitakushukuru na kukupigia pango kwa welekevu wako, Mungu wangu, nitakuimbia na kupiga zeze, wewe Mtakatifu wa Isiraeli.

23Midomo yangu inashangilia, kwa hiyo ninakuimbia, roho yangu inashangilia nayo, kwa maana umeikomboa.

24Nao ulimi wangu unausimulia wongofu wako mchana kutwa, kwani waliotafuta mabaya ya kunifanyizia huiva nyuso kwa soni.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help