1*Mimi ni mzabibu wa kweli naye Baba yangu ndiye mpalilizi.
2Kila tawi langu lisilozaa huliondoa; lakini kila tawi lizaalo hulitakasa akilipogoa, lipate kuzaa mengi.
3Ninyi mmekwisha kutakata mkilipokea lile Neno, nililowaambia.
4Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu! Kama tawi lisivyoweza kuzaa likiwa peke yake, lisipokaa mzabibuni, vivyo hivyo nanyi hamna mwezacho, msipokaa ndani yangu.
5Mimi ni mzabibu, ninyi m matawi. Anayekaa ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa mengi. Kwani pasipo mimi hamna mwezacho kukifanya.
9*Kama Baba alivyonipenda, ndivyo, nami ninavyowapenda ninyi. Kaeni na kunipenda!
10Mtakapoyashika maneno yangu mtakaa na kunipenda, kama mimi nilivyoyashika maagizo ya Baba yangu, nikakaa na kumpenda yeye.Upendano.
11Nimewaambia haya, furaha yangu iwakalie, nanyi furaha yenu itimie yote.
26*Lakini atakapokuja mtuliza mioyo, nitakayemtuma toka kwa Baba, yule Roho wa kweli atakayetoka kwa Baba, ndiye atakayenishuhudia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.