2 Mambo 31 - Swahili Roehl Bible 1937

Matambiko ya kimizimu yanaondolewa.

1Walipokwisha kuyamaliza hayo yote, Waisiraeli wote waliokuwako wakatoka kwenda zao katika miji ya Yuda, wakazivunja nguzo za kutambikia, wakaikatakata nayo miti ya Ashera, wakavibomoa vijumba vya kutambikia vilimani pamoja na meza zao za kutambikia katika nchi zote za Yuda na za Benyamini na za Efuraimu na za Manase, mpaka wakavitowesha kabisa hivyo vyote, kisha wana wote wa Isiraeli wakarudi kila mtu mahali palipokuwamali yake katika miji yao.Matengenezo mapya ya mambo ya watambikaji na ya Walawi.

2Kisha Hizikia akaweka kazi za zamu za watambikaji na za Walawi zizipasazo zamu zao, kila mtu akawa na kazi yake ya utumishi wake, watambikaji na Walawi: kuteketeza ng'ombe za tambiko na kutengeneza ng'ombe za tambiko za shukrani na kutumikia malangoni kwa matuo yake Bwana na kumshukuru na kumshangilia.

3Akayaweka nayo yampasayo mfalme kuyatoa katika mali zake kuwa ng'ombe za tambiko za asubuhi na za jioni na za matambiko ya siku za mapumziko na ya miandamo ya mwezi na ya sikukuu, kama ilivyoandikwa katika Maonyo ya Bwana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help