1Wafalme wote wa Waamori waliokaa ng'ambo ya huku ya Yordani upande wa baharini nao wafalme wote wa Wakanaani waliokaa pwani waliposikia, jinsi Bwana alivyoyapwesha maji ya Yordani mbele ya wana wa Isiraeli, mpaka waishe kuvuka, mioyo yao ikayeyuka, hakuwako mtu wa kwao asiyezimia roho kwa ajili ya wana wa Isiraeli.Kutahiri.
2Wakati huo Bwana akamwambia Yosua: Jitengenezee visu vya mawe makali, uwarudie wana wa Isiraeli kuwatahiri mara ya pili!
3Ndipo, Yosua alipojitengenezea visu vya mawe makali, akawatahiri wana wa Isiraeli katika Kilima cha Araloti (Tohara).
4Tena sababu yake Yosua ya kuwatahiri ilikuwa hii: watu wote waliotoka Misri waume wao wote walikuwa watu wa vita, nao walikufa nyikani njiani, walipokwisha kutoka Misri.
5Wale watu wote waliotoka walikuwa wametahiriwa, lakini wale watu wote waliozaliwa nyikani njiani, walipokwisha kutoka Misri, hawakutahiriwa.
6Kwani wana wa Isiraeli walizunguka nyikani miaka 40, mpaka wale watu wa vita wote pia waliotoka Misri walipokwisha kufa, kwa kuwa hawakuisikia sauti ya Bwana; kwa hiyo Bwana aliwaapia, wasiione ile nchi, yeye Bwana aliyowaapia baba zao, ya kama atatupa sisi, ni nchi hiyo inayochuruzika maziwa na asali.Yosua anatokewa na malaika.
13Ikawa, Yosua alipokuwa huko karibu ya Yeriko, akayainua macho yake na kuchungulia, mara akaona mtu aliyesimama hapo na kumtazama, namo mkononi mwake alishika upanga uliokwisha kuchomolewa. Yosua alipomwendea na kumwuliza: Wewe u mtu wa kwetu au wa adui zetu?
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.