Zakaria 12 - Swahili Roehl Bible 1937

Mungu atawaokoa Wayerusalemu na Wayuda.

1Tamko zito la Bwana, alilowaambia Waisiraeli. Ndivyo, asemavyo Bwana aliyezitanda mbingu, aliyeuweka msingi wa nchi, aliyeiumba roho ya mtu ndani yake:

2Mtaniona, nikiuweka Yerusalemu kuwa chano cha kuwalevya sana wao wa makabila yote wanaokaa na kuuzunguka; hata Wayuda watapatwa na mambo, Yerusalemu utakaposongwa.Kiagio cha Roho takatifu. Kumwombolezea, waliyemchoma.

10Wao walio wa mlango wa Dawidi nao wenyeji wa Yerusalemu nitawamiminia Roho ya kuhurumiana na ya kuombeana; ndipo, watakaponitazama, waliyemchoma. Kisha wataniombolezea, kama watu wanavyomwombolezea mwana wa pekee, nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama mtu anavyoona uchungu kwa ajili ya mwana aliyezaliwa wa kwanza.Yoe. 2:28; Yoh. 19:37; Ufu. 1:7.

11Siku hiyo maombolezo yatakuwa mengi mle Yerusalemu, kama maombolezo yalivyokuwa mengi mle Hadadi-Rimoni kule bondeni kwa Megido.

12Nao wenyeji wa nchi hii wataomboleza kila mlango peke yake: Walio wa mlango wa Dawidi peke yao, nao wanawake wao peke yao, walio wa mlango wa Natani peke yao, nao wanawake wao peke yao.

13Walio wa mlango wa Lawi peke yao, nao wanawake wao peke yao; walio wa mlango wa Simei peke yao, nao wanawake wao peke yao.

14Vivyo hivyo milango yote itakayokuwa imesalia, wao wa kila mlango peke yao, nao wanawake peke yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help