Marko 9 - Swahili Roehl Bible 1937

1Akawaambia: Kweli nawaambiani: Miongoni mwao wanaosimama hapa wamo wengine, ambao hawatakuonja kufa, mpaka watakapouona ufalme wa Mungu, ukiisha kuja kwa nguvu.

Yesu anageuzwa sura.(2-13: Mat. 17:1-13; Luk. 9:28-36.)

2Baada ya siku sita Yesu akamchukua Petero na Yakobo na Yohana, akapanda pamoja nao peke yao pasipo watu wengine juu ya mlima mrefu. Huko akageuzwa sura yake machoni pao,

3nazo nguo zake zikawa nyeupe sana, zikamerimeta; nchini hakuna fundi anayeweza kuzing'aza hivyo.

4Wakatokewa na Elia pamoja na Mose, wakawa wakiongea na Yesu.

5Petero akasema akimwambia Yesu: Mfunzi mkuu, hapa ni pazuri kuwapo sisi, na tujenge vibanda vitatu, kimoja chako, na kimoja cha Mose, na kimoja cha Elia!

6Kwani hakujua, alilolisema, kwa maana waliingiwa na woga mkubwa.

7Kisha hapo pakawa na wingu, likawatia kivuli, sauti ikatoka winguni kwamba: Huyu ndiye mwanangu mpendwa, msikilizeni yeye!Kijana mwenye pepo.(14-29: Mat. 17:14-21; Luk. 9:37-42.)

14Walipokuja kwa wanafunzi wakaona kundi la watu wengi lililowazunguka, hata waandishi walikuwapo wakibishana nao.

15Papo hapo kundi lote lilipomwona yeye, wakastuka, wakamwendea mbio, wakamwamkia.

16Akawauliza: Mnabishana nini nao?

17Mmoja wao wale watu wengi akamjibu: Mfunzi, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo wa ububu.

18Napo pote anapomkamata anamsukumasukuma kwa nguvu, naye hutoka pofu na kukereza meno, kisha mwili wake hunyauka. Nami nikawaambia wanafunzi wako, wamfukuze huyo pepo, lakini hawakuweza.

19Naye akawajibu akisema: Enyi wa kizazi kisichomtegemea Mungu! Nitakuwapo nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa, nilipo!

20Wakampeleka kwake; naye alipomwona, mara pepo akamkumba, akaanguka chini, akafingirika na kutoka pofu.

21Akamwuliza baba yake: Hivyo vimempata tangu lini? Akasema: Tangu utoto wake;

22mara nyingi humtupa motoni na majini, maana amwue. Lakini ukiweza kitu tusaidie ukituonea uchungu!

23Yesu akamwambia: Ukiweza kumtegemea Mungu! Yote huwezekana kwake anayemtegemea Mungu.Ukubwa.(33-50: Mat. 18,1-9; Luk. 9,46-50.)

33Wakafika Kapernaumu. Alipokuwa nyumbani akawauliza: Njiani mlibishana nini?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help