Mashangilio 70 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba msaada wa Mungu.(Taz. 40:14-17.)Kwa mwimbishaji. Wa Dawidi wa ukumbusho.

1Mungu, piga mbio, uniopoe! Bwana, pigambio, unisaidie!Sh. 38:1.

2Sharti wapatwe na soni wakiumbuliwa walioitafuta roho yangu. Sharti warudishwe nyuma na kutwezwa wao waliopendezwa na mabaya yaliyonipata mimi.

3Sharti warudi nyuma na kuona soni wale walioniambia: Weye! Weye!

4Sharti wachangamke na kufurahiwa wote wakutafutao! Waupendao wokovu wako waseme pasipo kukoma: Mkuu ni Mungu!

5Nami mnyonge, hata mkiwa; Mungu, piga mbio, unijie! Msaada wangu na wokovu wangu ndiwe wewe; wewe Bwana, usinikawilie!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help