1Haya ndiyo maamuzi, utakayoyaweka mbele yao:
7Mtu akimwuza mwanawe wa kike kuwa kijakazi, hatatoka utumwani, kama waume wanavyotoka.Maagizo yapasayo wenye kuwaumiza wenzao.
18Watu wakigombana, mmoja akimpiga mwenzake jiwe au konde, asife, ila augue tu na kulala kitandani,
19naye akipata kuinuka tena na kujiendea nje kwa kujiegemeza na mkongojo, basi, yule aliyempiga asipatwe na jambo lo lote, atamlipa tu siku za kukaa bure pasipo kufanya kazi, nayo mauguzi hana budi kuyalipa.
20Mtu akimpiga fimbo mtumwa wake au kijakazi wake, naye akifa papo hapo, anapomshika kwa mkono wake, sharti alipizwe.
21Lakini akiwapo baadaye siku moja au mbili, hatalipizwa, kwani ni mali yake yeye.
22Watu wakigombana, tena hapo wakipiga mwanamke mwenye mimba, nayo mimba yake ikiharibika pasipo kumtia ugonjwa, sharti atozwe fedha, kama mumewe yule mwanamke atakavyomtakia; hana budi kuzitoa zizo hizo, waamuzi watakazomwagiza.
23Lakini akipata kuumizwa zaidi, sharti umtoze roho kwa roho,
24jicho ka jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,3 Mose 24:19-20; 5 Mose 19:21; Mat. 5:38.
25kuugua kwa kuugua, kidonda kwa kidonda, vilio kwa vilio.
26Mtu akimpiga mtumwa au kijakazi wake jicho na kuliharibu, sharti ampe ruhusa ya kutoka utumwani kwa kumlipa hilo jicho.
27Hata akimvunja mtumwa au kijakazi wake jino, sharti ampe ruhusa kutoka utumwani kwa kumlipa jino.
28Ng'ombe akimkumba mwanamume au mwanamke kwa pembe zake, akifa, sharti huyo ng'ombe auawe kwa kupigwa mawe, nyama zake zisiliwe, lakini mwenye ng'ombe hana neno.
29Lakini kama huyo ng'ombe alikuwa akikumba watu tangu siku nyingi, naye bwana wake alikuwa ameonywa, lakini hakumwangalia huyo ng'ombe, naye akiua mwanamume au mwanamke, basi, huyo ng'ombe sharti auawe kwa kupigwa mawe, naye bwana wake hana budi kuuawa.1 Mose 9:5.
30Lakini akitozwa fedha tu za kujikomboa, sharti azitoe zote, anazotakiwa, ziwe makombozi ya roho yake.
31Ng'ombe akikumba mtoto wa kiume au mtoto wa kike kwa pembe zake, sharti ahukumiwe vivyo hivyo.
32Lakini ng'ombe akikumba mtumwa au kijakazi kwa pembe zake, mwenye ng'ombe sharti amlipe bwana wao fedha 30, naye ng'ombe sharti auawe kwa kupigwa mawe.
Maagizo ya kuangalia nyama wa kufuga wa wengine.33Mtu akiacha shimo wazi au akichimba shimo pasipo kulifunikiza, kisha ng'ombe au punda akitumbukia humo,
34mwenye shimo sharti alipe fedha za kumrudishia yule bwana mali zake, kisha nyama aliyekufa atakuwa wake.
35Ng'ombe wa mtu akimkumba ng'ombe wa mwenzake kwa pembe zake, akafa, basi, watamwuza yule ng'ombe aliye mzima, lakini fedha, watakazozipata, sharti wazigawanye, naye ng'ombe aliyekufa sharti wamgawanye.
36Lakini kama ilikuwa imejulikana, ya kuwa huyo ng'ombe hukumba kwa pembe zake tangu siku nyingi, naye bwana wake hakumwangalia, sharti alipe ng'ombe aliye mzima mahali pake al iyekufa, kisha huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa wake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.